Home Habari za michezo JAMBO LA PHIRI BADO NDANI YA SIMBA….KAULI YA KLABU IMESIMAMIA UPANDE HUU…

JAMBO LA PHIRI BADO NDANI YA SIMBA….KAULI YA KLABU IMESIMAMIA UPANDE HUU…

Habari za Simba

Licha ya mshambuliaji wa Simba Moses Phiri kuongozana na wenzake katika kambi ya Dubai hajaweza kufanya mazoezi ya pamoja mpaka atakaporejeshwa hospitali kwa ajili ya vipimo zaidi.

Desemba 21 mwaka jana, Phiri aliumia katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar uliowapa wekundu hao pointi moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1.

Mkuu wa idara ya Simba, Ahmed Ally amesema jana kuwa, staa huyo yupo kambini lakini kuhusu afya yake bado haijatengamaa kujumuika na wenzake na awali baada ya vipimo alionekana kuwa fiti baada ya siku 10 lakini zimepita na staa huyo bado analalamika kutokuwa vizuri.

“Mchezaji anasema anasikia maumivu bado katika mguu wake, hivyo dokta atamwangalia zaidi ili kubaini tatizo ambalo bado linamsumbua,”alisema Ahmed. Kuhusu kambi alisema, kila mchezaji amefurahia mazingira hivyo anaamini benchi la ufundi litapata kitu katika siku hizo walizokaa huko.

Mbali na Phiri pia beki wao Henock Inonga aliyeumia mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao Simba ilishinda mabao 7-1 Desemba 30 naye anaendelea na matibabu huku Peter Banda akirejea.

SOMA NA HII  MIQUISSONE AIWEKEA NGUMU SIMBA....AGOMA KUPUNGUZA MSHAHARA WAKE...