Home Habari za michezo KISA USHINDI WA MAN UTD DHIDI YA MAN CITY…DUNIA NZIMA YAZIZIMA KWA...

KISA USHINDI WA MAN UTD DHIDI YA MAN CITY…DUNIA NZIMA YAZIZIMA KWA FURAHA..

Man UTD vs Man City

Hatimaye! Baada ya unyonge wa kupoteza mechi tatu mfululizo kuanzia mwaka juzi, Man United imefuta uteja baada ya kuibamiza Man City kichapo cha mabao 2-1.

Man United imepata ushindi huo kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa katika dimba la Old Trafford kuanzia saa 9:30 mchana.

Man City ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia jack Grealish aliyefunga dakika ya 60 baada ya kuingia akitokea benchi.

Man United ikajipanga na kurudisha bao la kwanza kupitia kwa Brundo Fernandes dakika ya 78 kabla ya Murcus Rashford kufunga bao lapili dakika ya 82 kwa pasi kali ya Alejandro Garnacho.

Ushindi huo umeifanya Man United kupanda hadi nafasi ya tatu nyuma ya Man City ikiwa na alama 38 na inakuwa na utofauti wa alama sita dhidi ya vinara Arsenal.

Mechi ijayo Man United itakutana na Crystal Palace January 18, ugenini wakati Man City ikikutana na Tottenham January 19.

Mballi na kuisogeza Man UTD mpaka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, Ushindi wa timu hiyo umeifanya dunia nzima kuzizima haswa kwa wapenzi wa timu hiyo.

Taarifa kutoka kila kona ya dunia zimeripotiwa kuwa mashabiki wa Man UTD wamejawa na furaha isiyo mithilika kama ilivyokuwa Argentina baada ya kutwa kombe la dunia nchini Qatar.

SOMA NA HII  KUHUSU MICHO KUMRITHI NABI JANGWANI...KIGOGO YANGA AFUNGUKA A-Z JINSI ISHU ILIVYO....