Home Habari za michezo RASMI…YANGA WATHIBITISHA KUACHANA NA BUMBULI….HUYU HAPA MTANGAZAJI WA AZAM TV ANAYETAJWA KUMRITHI…

RASMI…YANGA WATHIBITISHA KUACHANA NA BUMBULI….HUYU HAPA MTANGAZAJI WA AZAM TV ANAYETAJWA KUMRITHI…


Uongozi wa klabu ya Yanga, kupitia kwa Kaimu Mtendaji wake Mkuu, Simon Patrick umethibitisha kuachana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Hassan Bumbuli.

Kwa mantiki hiyo sasa, nafasi hiyo iko Wazi na wenye Sifa wanaruhusiwa kutuma maombi.

Kuachana kwa Bumbuli na Klabu ya Yanga, ni kukamilisha tetesi zilizoanza kuvuma siku chache zilizopita kuwa BUmbuli ametemwa klabuni hapo.

Pamoja na Mshereheshaji maarufu nchini Taji Liundi kukaimu nafasi ya Bumbuli wakati wa maandalizi ya Siku ya Wananchi, Mchambuzi na mtangazaji wa Azam TV, Ally Kamwe anatajwa kuwa miongoni mwa watu watakaopewa nafasi hiyo.

Bumbuli ni miongoni mwa waliokuwa waajiriwa wa Yanga wakati wa utawala wa Dk Mshindo Msola ambapo mara baada ya kuingia utawala mpya wa Injinia Hersi Saidi, mabadiliko mengi yalifanyika ikiwemo aliyekuwa Mtendaji Mkuu Senzo Mbatta ambaye aliondoka mara baada ya mkataba wake kuisha.

SOMA NA HII  KAGERA SUGAR WAIANDALIA SIMBA GARI LA KUBEBA WAGONJWA...OKWI NA KASEJA WATAJWA...