Home Habari za michezo SAMATTA AFUNGUKA ‘ALIVYOJIKAZA KISABUNI’ NA PESA ZA TP MAZEMBE…ADAI ANGEKUWA CHIZI…

SAMATTA AFUNGUKA ‘ALIVYOJIKAZA KISABUNI’ NA PESA ZA TP MAZEMBE…ADAI ANGEKUWA CHIZI…

Samatta

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania na mchezaji wa Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samata wakati akifanyiwa mahojiano na Salam Jabir kwenye kipindi cha Salama Na.. amesema angeweza kuchanganyikiwa kutokana na kushika pesa nyingi akiwa mdogo.

Salama Jabir: Samatta unasifika sana kuwa na heshima kwa kila mtu, nani amekufundisha hiyo?

Samatta: “Siamini kama nilipaswa kufundishwa, naamini ni jinsi nilivyo ni kitu ambacho sijajifunza nilizaliwa nacho.

Katika umri mdogo ningeweza kuwa chizi kwa sababu nimeenda TP Mazembe nikiwa na umri mdogo (Teneger age), ningeweza kuchanganyikiwa kwa malipo ambayo nilikuwa nayapata TP Mazembe ningweza kuvurugukiwa kwa asilimia kubwa ya vijana ambao nawajua wangeweza kuwa na maisha tofauti,” amesema Mbwana Samatta.

Itakumbukwa kuwa Samatta, kabla ya kujiunga na TP Mazembe aliichezea Simba akitokea African Lyon iliyokuwa ikifahamika kama Mbagala Marketi.

Mchezo mmoja wa hatua ya kuwania kufuzu makundi ligi ya mabingwa Afrika katika ya Simba na Tp Mazembe, ulitosha kuwashawishi wa Congo kulipa dola 150,000 kumsajili mchezaji huyo ambaye nyakati hizo alikuwa machachari.

Baada ya kutua TP Mazembe, Samatta alifanikiwa kushinda mataji mengi ya ligi ya Congo pamoja na lile la Ligi ya Mabingwa Afrika huku akitajwa pia kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa Ligi za Ndani kwa mwaka 2015.

Kutoka hapo safari ya Samatta kwenye soka ikahamia nchini Ubelgiji ambapo alisajiliwa na KRC Genk ambapo nako aliuwasha moto kisawasawa hali iliyompelekea kusajliwa na Aston Villa ya Uingereza .

Akiwa hapo, Samatta alisaini dili la kuichezea timu hiyo kwa mkataba wa miaka minne, huku ikisemekana alikuwa akilipwa zaidi ya milioni 80 kwa wiki.

Baada ya kucheza msimu mmoja akiwa hapo, ambao haukuwa msimu mzuri kwake, alisajiliwa na Timu ya Uturuki, kabla ya hivi karibuni kurudi tena Genk kwa mkopo.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTUA BONGO NA KUIONA YANGA INAVYOCHEZA..CHICO AKUNA KICHWA WEE..KISHA ANENA HAYA...