Home Habari za michezo WAKATI MAYELE AKIWEKA REKODI CAF…NABI NAYE KAWEKA REKODI HII YA KIBABE TOKA...

WAKATI MAYELE AKIWEKA REKODI CAF…NABI NAYE KAWEKA REKODI HII YA KIBABE TOKA ATUE YANGA…


Takwimu zinaonyesha Fiston Mayele anakuwa mchezaji wa tatu kufunga hat trick kwenye mashindano ya CAF kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara ndani ya kipindi cha miaka nane kuanzia mwaka 2014.

Hii ni baada ya kuifunga Zaalan FC ya Sudan Kusini bao 3 katika mchezo wa jana Septemba 10, 2022, hqtua ya awali ya mtoano klabu Bingwa Afrika ambapo Yanga wakiwa ugenini katika Dimba la Mkapa waliibuka na ushindi wa bao 4-0.

Ikumbukwe kuwa, Mrisho Khalfan Ngassa akiwa Yanga, alifunga hat trick dhidi ya Komorosine mwaka 2014 katika michuano kama hiyo ya Klabu Bingwa Afrika.

Aidha, Kipre Tche Tche akiwa Azam alifunga hat trick dhidi ya Bidvest Wits Mwaka 2016 katika dimba la Azam Complex pale Chamazi. Na hawa Bidvest ndio walikuwa Mabingwa wa Afrika Kusini msimu huo.

Rekodi nyingine aliyoiweka Mayele jana ni kufunga hat trick yake ya kwanza katika mechi za mashindano akiwa na Yanga.

Pia, ndiyo mechi ya kwanza ya kimataifa kwa Kocha Nasreddine Nabi kushinda tangu ajiunge na Yanga mwaka 2021.

SOMA NA HII  CHAMA RASMI NI MALI YABRS BERKANE YA MOROCCO