Home Uncategorized KOCHA LIPULI: WACHEZAJI WALIKUWA HAWAFANYI MAZOEZI

KOCHA LIPULI: WACHEZAJI WALIKUWA HAWAFANYI MAZOEZI


NZEYIMANA Mailo, Kocha Mkuu wa Lipuli FC amesema kuwa wachezaji wake hawakuwa wakifanya mazoezi wakati wa mapumziko ya lazima yaliyosababishwa na janga la Virusi vya Corona.

Mei 31, Lipuli iliwasili kambini na kuanza kufanya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi, Juni 13.

Masuala ya michezo yalisimamishwa Machi 17 na Serikali baada ya kuibuka kwa janga la Corona na Serikali imeridhia masuala ya michezo kuendelea kwa kile ilichoeeza kuwa maambukizi yamepungua.

Mailo amesema:”Wachezaji wangu walikuwa hawafanyi mazoezi ndani ya Lipuli jambo ambalo limefanya nianze kuwasimamia upya kuweza kuwarejesha kwenye ubora wao.

“Ninaona wanafanya vizuri kwa kuwa tumeanza nao mazoezi wakati huu kwa pamoja tutafanya vizuri kwani ninajua namna ya kwenda nao sawa kikubwa nimewaambia wanapaswa wajitume,” amesema.

SOMA NA HII  POLISI TANZANIA WATAJA SABABU YA KUKAZA NDANI YA LIGI KUU BARA