Home Simba SC CHAMA KUIBUKIA MOROCCO MSIMU UJAO,AJIFUNGA MIAKA MITATU

CHAMA KUIBUKIA MOROCCO MSIMU UJAO,AJIFUNGA MIAKA MITATU


 CLATOUS Chama kiungo namba moja kwa kutengeneza pasi za mwisho anatajwa kujiunga na Klabu ya RS Berkane ya Morocco kwa dili la miaka mitatu.


Timu hiyo inanolewa na Kocha Mkuu, Florent Ibenge ambaye alikuwa anafundisha AS Vita anatambua vema uwezo wa Chama kwa kuwa alikutana naye kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

Ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 nyota huyo alitengeneza jumla ya pasi 15 na alifunga mabao nane akiwa ni namba moja kwa utengenezaji wa pasi ndani ya ligi.

Taarifa zimeeleza kiungo huyo hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kwa msimu ujao wa 2021/22.

Mbali na Chama pia nyota wao Luis Miquissone yupo kwenye hesabu za mwisho kutua nchini Misri kwa ajili ya kujiunga na Klabu ya Al Ahly ya Misri.

Tayari jezi namba 11 ambayo aliyokuwa anavaa Luis amekabidhiwa kiungo mpya Peter Banda ambaye anatajwa kuwa mbadala wa nyota huyo.

Simba imeweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22 ambapo Luis hakuwa sehemu ya kikosi hicho ambacho kipo kambini. 

SOMA NA HII  BAADA YA 'KUPIGWA ZA USO' MECHI TATU ZIZLIZOPITA...MGUNDA KAANZA KULIA UGUMU WA LIGI....