Home Habari za michezo CAF WALIVYOIPELEKA ‘DABI’ YA SIMBA NA YANGA ALGERIA…SHOW NZIMA ITAKUWA HIVI…

CAF WALIVYOIPELEKA ‘DABI’ YA SIMBA NA YANGA ALGERIA…SHOW NZIMA ITAKUWA HIVI…

HABARI ZA SIMBA NA YANGA

Kwa mara ya kwanza, timu za Simba na Yanga zitakuwa nchini Algeria kwa wakati mmoja (ndani ya wiki moja) kwenye mechi za michuano ya CAF, kila timu ikiwa na kibarua chake.

Wiki hiyo ni ile yenye tarehe 6-8 mwezi Desemba mwaka huu, ambapo Simba itakwenda kucheza mchezo wa raundi ya pili hatua ya makundi Kombe la Shirikisho dhidi ya CS Costantine ambayo maskani yake ni katika mji wa Costantine…. Wakati Yanga ikiwa Algiers kucheza dhidi ya MC Alger, mchezo wa hatua hiyohiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika…

Mechi hizi huenda zikapishana kwa siku moja hadi mbili lakini pia huenda zikepigwa katika miji tofauti ambayo ni Costantine na Algiers.

Je, Simba na Yanga ‘kuivamia’ Algeria kwa wakati mmoja kusaka alama tatu za CAF, unapata picha gani????

Ratiba ya Simba iko hivi:-

28/11/2024: Simba vs Bravos.
08/12/2024: Costantine vs Simba.
15/12/2024: Simba vs Sfaxien.
05/01/2025: Sfaxien vs Simba.
12/01/2025: Bravos vs Simba.
19/01/2025: Simba vs Costantine.

Ratiba kamili ya yanga iko hivi:-
26/11/2024: Yanga vs Al Hilal.
06/12/2024: MC Alger vs Yanga
13/12/2024: TP Mazembe vs Yanga
03/01/2025: Yanga vs TP Mazembe
10/01/2025: Al Hilal vs Yanga
17/01/2025: Yanga vs MC Alger.

SOMA NA HII  IBRAHIM 'BACCA'..UNAAMBIWA MPAKA CHIPS KAUZA...AFUNGUKA 'MASHOGA' KUMSUMBUA INSTA...