Home Uncategorized SIMBA WAIPOTEZA YANGA KWA PACHA WA MWAMNYETO JUMLAJUMLA

SIMBA WAIPOTEZA YANGA KWA PACHA WA MWAMNYETO JUMLAJUMLA


IBRAHIM Ame, beki anayekipiga ndani ya Coastal Union inaelezwa kuwa amemalizana na mabosi wa Simba ambao walikuwa wakisaka saini ya Bakari Mwamnyeto ambaye ameibukia ndani ya Yanga.

 Yanga ilikuwa kwenye mazungumzo ya mwisho kupata saini ya Ame ila kwa kuwa waliizidi ujanja Simba wakaamua kuwajibu kibabe kwa kumalizana na beki huyo.

Wote wawili ndani ya Coastal Union walikuwa na maelewano mazuri ila bosi alikuwa Mwamnyento ambaye alikuwa ni nahodha wa Coastal Union.

Ikiwa imemaliza nafasi ya 7 kwenye msimamo imefungwa jumla ya mabao 30 ambayo ni machache kuliko yale iliyofungwa Namungo iliyo nafasi ya nne ikiwa imefungwa mabao 37.

Habari kutoka ndani zinaeleza kuwa tayari Ame yupo kwnye ardhi ya Dar tayari kumalizana na mabosi wa Msimbazi.

SOMA NA HII  ISHU YA SIMBA KUSHINDA DAKIKA ZA USIKU, SVEN ATAJA SABABU