Home Habari za michezo SKUDU AVUNJA UKIMYA YANGA….AFUNGUKA A-Z KINACHOMKWAMISHA…

SKUDU AVUNJA UKIMYA YANGA….AFUNGUKA A-Z KINACHOMKWAMISHA…

Habari za Yanga leo

WINGA wa Yanga, Mahlatse Makudubela (Skudu), ameweka wazi juu anaendelea kupambania namba kwenye kikosi cha Yanga kumshawishi kocha Miguel Gamondi anavyompa nafasi kuonyesha kiwango kizuri

Amesema ameshindwa kupata nafasi ndani ya kikosi cha kwanza kulingana na ushindani uliopo lakini hawezi kukata tamaa kwa sababu anapata nafasi ya kucheza na kutakiwa kuonyesha kitu.

Skudu amesema anaimani na kiwango chake bado yupo vizuri kwa ajili ya kusaidia Yanga kufikia malengo yao ya kutetea mataji yao ya michuano ya ndani na kufanya vizuri kimataifa.

“Ni kweli ushindani wa namba ni mkubwa, kikubwa nitapambana kuhakikisha kufanya vizuri na kusaidia Yanga inafanikiwa kupata matokeo chanya, ninaimani nitaonyesha kiwango kizuri kila ninapopata nafasi ya kucheza.

Mashabiki wa Yanga wanapenda mpira jambo ambalo naliona ni zaidi ya familia kuicheza timu hii na niwaambie tu kuwa nitapambana kwa ajili ya kuyapata mafanikio makubwa zaidi na kuweka historia nyingine,” amesema Skudu.

Ameongeza kuwa anaendelea kuongeza juhudi katika uwanja wa mazoezi na mechi ambayo akipewa nafasi na kufikia malengo yanayotarajiwa na Wananchi.

SOMA NA HII  ILE ISHU YA MATOLA KUSEPA....UONGOZI SIMBA WAIBUKA NA TAMKO HILI..

1 COMMENT