Home Habari za michezo BAADA YA USHINDI WA MBINDE JANA….GAMONDI KAFUNGA MACHO KISHA AKASEMA HILI…

BAADA YA USHINDI WA MBINDE JANA….GAMONDI KAFUNGA MACHO KISHA AKASEMA HILI…

Habari za Yanga SC

BAADA ya ushindi na kurejea kileleni kwa alama 34, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema ana matarajio makubwa ya kuendelea vizuri katika mbio za kutetea taji lao la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu huu.

Gamondi aliongea hayo baada ya kukamilika kwa dakika 90 za mchezo wa ligi hiyo , Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0 Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Bao pekee la ushindi limefungwa na Mudathir Yahya dakika ya 86 akitumia pasi ya Kibabage, wote wawili walitokea benchi kipindj cha pili ambapo Dodoma Jiji walikuwa wanakaribia kupata pointi moja, mpango ukavurugwa jioni.

Yanga inarejea nafasi ya kwanza ikiwashusha Azam FC mpaka nafasi ya pili huku Simba ikiwa nafasi ya tatu, pointi 34 imekusanya baada ya kucheza mechi 13 sawa na Azam FC iliyo nafasi ya pili na pointi 31 huku Simba ikiwa nafasi ya tatu na pointi 26 baada ya kucheza mechi 11.

Gamondi amesema anawapongeza wachezaji wake, wamecheza vizuri tofauti na mechi ya kwanza na Kagera Sugar ambao walishindwa kupata matokeo na safari hii wamecheza vizuri na kupata ushindi ambao unawareness kileleni.

Amesema kulingana na ugumu wa ligi anaimani kubwa ya timu yake inaweza kutetea taji hilo la ubingwa kwa msimu huu kwa sababu ana kikosi imara licha ya kuwakosa baadhi ya nyota wake wengine akiwemo Djigui Diarra na Stephen Aziz Ki.

“Tulikosa wachezaji wetu, lakini waliokuwepo walifanya vizuri, wametoka katika mapumziko na wanatakiwa kurejea taratibu tulikosa alama mechi iliyopita na sasa tukacheza vizuri na kufunga dakika za mwishoni.

Kipindi cha kwanza tulitengeneza nafasi na kushindwa kuzitumia lakini mwishoni tukaweza kutumia nafasi na kuvuna alama tatu muhimu mbele ya wapinzani wetu ambao walikuwa wakipoteza muda,” amesema Gamondi.

Kiungo Mudathiri ambaye alifunga bao pekee la ushindi, amesema alipewa maelekezo na kocha wake (Gamondi) kuwa anatakiwa kupanda na kushuka na anakuwa makini na nafasi zinazopatikana na kupata bao.

“Nilitamani sana kufunga hii mechi, kocha alinipa maelekezo na nimeenda kuyafanyia kazi kwa kile nilichoambiwa kwa kufanya majukumu yangu ya kuhakikisha naenda kushambulia na kuhakikisha nazuia, tulifanikiwa na kupata bao la ushindi kwa kuvuna pointi tatu muhimu, “ amesema Mudathiri.

SOMA NA HII  JAMA JAMA LITAKUFA JITU AISEEE....KWA SIMBA HII IJAYO WEKA MBALI NA WATOTO...MO DEWJI HATAKI MASIKHARA KABISA...