Home Uncategorized HAO GWAMBINA WAPANIA KUPANDA LEO, RAMANI IPO NAMNA HII

HAO GWAMBINA WAPANIA KUPANDA LEO, RAMANI IPO NAMNA HII


MOJA ya timu ambazo zina uhakika wa kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao wa 2020/21 ni Gwambina FC ya Mwanza kutokana na hesabu zake kuelekea kutiki kwa sasa.
Ikiwa chini ya Kocha Mkuu Furjems Novatus sambana na Athuman Bilali imekuwa kwenye ubora wake ambapo kwa sasa ipo nafasi ya kwanza na pointi zake 40 baada ya kucheza mechi 18.
Imewaacha kwa tofauti ya pointi 10, Geita Gold iliyo nafasi ya pili ikiwa na pointi 30 nayo pia imecheza mechi 18.
Imebakiza mechi nne kukamilisha mzunguko wa pili ili kukata tiketi yake ya kushiriki ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo inahitaji pointi tatu kujiwekea ufalme wao ndani ya Ligi Kuu Bara.
Mechi nne ilizobakiwa nazo ni dhidi ya Transit Camp,Pamba FC,Rhino Rangers na Mashujaa na uwanja wake wa nyumbani ni Gwambina Complex ambao ni wa kisasa.
Leo Uwanja wa Uhuru itamenyana na Transit Camp iwapo itashinda itapanda Ligi Kuu Bara ikiwa na mechi tatu mkononi.

Mkuu wa Idara ya Mashindano ndani ya Gwambina FC, Mohamed Moshi Almas maarufu kama Mtabora ambaye anafunguka mengi kuhusu ramani za ushindi, huyu hapa:-
“Awali nilikuwa nje ya timu nikiwa ni mshauri tu ila rasmi nilianza kazi Oktoba 24, nakumbuka niliikuta timu ikiwa nafasi ya tano baada ya kucheza mechi nane na pointi zake zilikuwa 12.
“Wakati huo kinara alikuwa ni Geita Gold ambaye alikuwa na pointi 17 alituacha kwa pointi tano.  
Kipi kimeweza kuitoa nafasi ya tano mpaka ya kwanza?
“Hesabu kubwa ilikuwa ni kuona kwamba yale mambo ambayo hayaendi sawa yanaisha. Unajua unapozungumzia uongozi ni falsafa ya mtu hivyo tulichokubaliana kwa pamoja ni kuvunja yale matabaka na kuweka umoja katika kila jambo.
Malengo makubwa kwa sasa ni yapi?
“Kuona timu msimu ujao inashiriki Ligi Kuu Bara tena tunahitaji ikamilike hivyo tukiwa na mechi mkononi kwani kwa sasa tunahitaji pointi tatu pekee ambazo tumezifuata Dar es Salaam kwa wana Transit Camp, Juni 20, Uwanja wa Uhuru.
Unautazameje huo mchezo?
“Walimu wanajua na wachezaji pia wanatambua kwani tunatambua kwamba ushindi wetu utatufanya tufikie malengo yale ambayo tumeyaweka. Tumeongea na wachezaji wamekubali kuendelea ile kasi ambayo tulikuwa nayo kabla ya kuibuka kwa janga la Corona.
Ugumu kwenye mpira na uongozi upo wapi?
“Kufikia yale ambayo unayatarajia kwani muda mwingine mambo huwa yanakwenda vile yanavyotaka na sio unavyotaka wewe.Pia unaweza kukata tamaa lakini hiyo sio njia nzuri kwa kiongozi.
Kasi ya Gwambina inabebwa na nini?
“Mpira mgumu, unahitaji matokeo muda mwingine ila kikubwa ni kutimiza majukumu ya wachezaji pamoja na ushirikiano.
Ishu ya kununua mechi ipoje kwa mechi za nyumbani?
“Hilo wengi wanasema ila ukweli ni kwamba ili ushinde ni lazima kuwe na mipango ya kiufundi. Wachezaji wawe tayari kufanya kazi na kuwa na moyo mmoja katika kile ambacho wanakifanya.
Kulikuwa na mpango gani muda ule wa kupambana na Corona?
“Tunamshukuru Mungu, wachezaji walikuwa na program ya kufanya na tuliendelea kuchukua tahadhari ili kuwa salama kwa kuwa muhimu kuamini kwamba bado tunapaswa kuendelea kuchukua tahadhari,” anamaliza Mtabora
Hizi hapa rekodi zake akiwa kiongozi:-
Mechi zake za Ligi Daraja la Kwanza mpaka sasa akiwa kwenye uongozi zimechezwa jumla ya mechi 11 ambapo Gwambina ilishinda mechi 10 na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Stand United.
Hizi hapa za ushindi:-Mechi 10 ambazo Gwambina ilishinda kwenye Ligi Daraja la Kwanza ikikusanya mabao 23 na kufungwa mabao 7 hizi hapa:-Gwambina 3 -1 Transit Camp, Gwambina 1-0 PambaRhino Rangers 1-2 Gwambina, Mashujaa 0-1 Gwambina.
 Arusha FC 1-3 Gwambina, Gipco 1-2 Gwambina,Gwambina 1-0 Geita GoldGwambina 3-1 Sahare All Star, Gwambina 4-0 Mawenzi Market, Green Warriors 1-3 Gwambina.

SOMA NA HII  KIUNGO HUYU MTIBWA SUGAR YUPO TAYARI KUIBUKIA YANGA

Kombe la Shirikisho pia Gwambina ilipambana ila iliishia hatua ya 16 bora baada ya kuchapwa bao 1-0 na Yanga Uwanja wa Uhuru. Ilishinda mechi mbili,ilikuwa:-Gwambina 3-0 Mbeya Kwanza, Gwambina 1-1 Ruvu Shooting
ila ilishinda kwa Penalti tisa kwa nane.

Mechi saba za kirafiki ambapo Gwambina ilishinda mechi sita na sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Kagera Sugar. Hizi hapa ilishinda:-Gwambina 2-1 MbaoToto Africa 1-3 Gwambina,
Gwambina 5-0 Bifad FC, Mwanza Combain 2-5 GwambinaGwambina 1-0 AllianceGwambina 1-0 Kagera.