Home Habari za michezo WAKATI MECHI YA SIMBA vs YANGA IKIPANGWA KUCHEZWA CCM KIRUMBA…GEITA GOLD KUISAIDIA...

WAKATI MECHI YA SIMBA vs YANGA IKIPANGWA KUCHEZWA CCM KIRUMBA…GEITA GOLD KUISAIDIA SIMBA….


Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ limetangaza Ratiba ya Michezo ya Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ msimu huu 2021/22.

TFF imetoa Ratiba ya Michezo hiyo leo Jumatatu (Mei 16) kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, huku Simba SC ikiwa timu ya mwisho kutinga katika hatua hiyo kwa kuifunga Pamba FC kutoka Mwanza mabao 4-0 juzi Jumamosi (Mei 14).

Mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho unaonyesha Young Africans itakutana na Mtani wake wa Jadi Simba SC katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Jumamosi (Mei 28).

kabla ya mchezo huo, Simba SC itakua na faida ya kuzoea mazingira ya jiji la Mwanza, kufuatia Ratiba ya Ligi Kuu kuonyesha itakua na mchezo dhidi ya Geita Gold FC Jumapili (Mei 22), katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Young Africans itakua Dar es salaam ikicheza dhidi ya Mbeya Kwanza FC katika Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi (Mei 21), hivyo baada ya hapo italazimika kuanza safari ya Mwanza tayari kwa mchezo huo.

Mchezo wa pili wa Nusu Fainali utazikutanisha Azam FC ya Dar es salaam dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha Jumapili (Mei 29).

Hii ni mara ya pili kwa michezo ya Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ kuchezwa katika viwanja huru, ambapo msimu uliopita viwanja vya Alli Hassan Mwinyi (Tabora) na Majimaji (Songea-Ruvuma) vilitumika.

Young Africans ilikutana dhidi ya Biashara United Mara katika Uwanja wa Alli Hassan Mwinyi Tabora, huku Simba SC ikipapatuana na Azam FC Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.

Fainali ya msimu uliopita ilipigwa Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here