Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA MBRAZILI KUFUKUZWA….KIGOGO SIMBA AVUNJA UKIMYA…ATAJA MSIMAMO YA KLABU…

KUHUSU ISHU YA MBRAZILI KUFUKUZWA….KIGOGO SIMBA AVUNJA UKIMYA…ATAJA MSIMAMO YA KLABU…

Habari za Simba

Baada ya kutinga katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), Klabu ya Simba SC imeweka wazi kuwa, inaamini kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’, atawafikisha mbali msimu huu.

Pia, Simba SC imesema ina imani Robertinho atatimiza malengo ambayo klabu imempa katika michuano ya ndani na kimataifa.

Simba SC yenye maskani yake Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es salaam, mwanzoni mwa msimu ilijiwekea malengo ya kutwaa mataji yote ya ndani na kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu.

Hadi sasa, Mbrazili huyo ameiongoza timu hiyo kutwaa Ngao ya Jamii na kuipeleka katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Simba SC ilitinga makundi ya michuano hiyo kwa kuitoa Power Dynamos ya Zambia kwa sheria ya bao la ugenini baada ya kutoka sare ya mabao 3-3.

Timu hiyo ilitoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Zambia, kabla ya juzi Jumapili (Oktoba Mosi) kulazimisha sare ya bao 1-1 katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Pamoja na kutinga makundi, baadhi ya mashabiki wa Wekundu hao wa Msimbazi walionyesha kutoridhishwa na kiwango cha kikosi cha Robertinho.

Hata hivyo, Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Iman Kajula amesema uongozi wa Simba SC unaamini Robertinho ataipa mafanikio makubwa timu hiyo msimu huu.

Kajula amesema wamewasikia baadhi ya mashabiki wakionyesha kutoridhishwa na kiwango cha timu chini ya kocha huyo, lakini klabu bado ina imani na Robertinho.

“Unajua mashabiki wanapenda kuzungumza hivyo huwezi kufuatisha kila jambo wanalosema, sisi bado tutaendelea kupata huduma ya Robertinho,” amesema

Mtendaji huyo aliongeza kuwa: “(Mashabiki) watulie na wampe muda kwani naamini timu yetu bado inajenga kwa kuwa ina wachezaji wengi wapya, naamini siku za mbele itafanya vizuri zaidi.”

SOMA NA HII  BENCHIKHA AFUNGUKA HALI HALISI YA KIKOSI CHA SIMBA UPANDE HUU