Home Habari za michezo BENCHIKHA AFUNGUKA HALI HALISI YA KIKOSI CHA SIMBA UPANDE HUU

BENCHIKHA AFUNGUKA HALI HALISI YA KIKOSI CHA SIMBA UPANDE HUU

Habari za Simba

Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha amesema anaridhishwa na uimara wa safu yake ya ulinzi ambayo anaona imeimarika kwa asilimia 70 mpaka sasa kulinganisha na alivyoikuta wakati akichukua mikoba ya kuifundisha timu hiyo.

Katika mechi tatu ambazo ameiongoza timu hiyo tangu kuchukua nafasi ya Roberto Oliviera ‘Robertinho’, Simba imeruhusu bao moja pekee kwenye kipigo cha bao 1-0 nyumbani kwa Wydad Casablanca kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika, lakini iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na ushindibwa bao 2-0 dhidi ya Wydad kwa Mkapa.

Benchikha amewapongeza wachezaji wake hasa safu ya ulinzi kwa kuonyesha mabadiliko makubwa ya kiuchezaji tofauti na awali ambako takribani kila mchezo walikuwa wakiruhusu bao

Benchikha amesema ameridhishwa kuona timu yake haijaruhusu goli kwenye mchezo wa juzi na kwamba walikuwa na nafasi ya kupata ushindi mkubwa zaidi lakini wameangushwa na uwanja ambao haukuwa rafiki na kuwanyima nafasi ya kucheza soka safi lakini hata hivyo amefurahishwa na kile wachezaji wake walichokifanya.

Alieleza kuwa Wydad ni timu nzuri na walitoa ushindani mkubwa lakini wao walikuwa bora katika kila eneo ikiwemo safu ya ulinzi ambayo hawajaruhusu wapinzani wao kupata bao na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-0.

“Tulicheza vizuri sana.., nawapongeza wachezaji wangu, tulimiliki sehemu kubwa ya mchezo lakini uwanja haukuwa rafiki na kutunyima kucheza soka safi, Wydad ni timu kubwa Afrika, ina wachezaji wazuri na wanacheza soka safi lakini na sisi tulikuwa bora ndio maana tumepata ushindi,” alisema Benchikha.

Aliongeza kuwa ameridhishwa na jinsi safu yake ya ulinzi inayounda na Henock Inonga, Che Malone, Mohammed Zimbwe Shomari Kapombe na kipa Ayoub Lakred kuwa makini na anaimani kubwa kwenye michezo ijayo watafanya vizuri zaidi.

“Mpira ni mashabiki, kwetu wa nafasi kubwa sana katika kutusaidia kufanya vizuri, tunaomba wajitokeze kwa wingi na kuendelea kutusapoti, tunawaahidi tutaonyesha soka safi, tunaka ushindi tu,” alisema Benchikha.

SOMA NA HII  YANGA YAREJEA DAR NA POINTI MBILI, HESABU ZAKE NI KWA GWAMBINA