Home Uncategorized GADIEL MICHAEL AWAANGUKIA VIONGOZI NA MASHABIKI WA YANGA

GADIEL MICHAEL AWAANGUKIA VIONGOZI NA MASHABIKI WA YANGA


GADIEL Michael, bieki mpya wa Simba ambaye amesaini kandarasi ya miaka miwili akitokea Yanga amewaomba radhi viongozi wa Yanga na mashabiki wake.

Kupitia ukurasa wa Instagram, Michael ameandika namna hii:-
“Wakati mwingine mtu unalazimika kufanya maamuzi yako peke yako kwa sababu anaewajibika na maisha yako mwisho wa siku ni mtu mwenyewe.

 “Mpira ndio kazi yangu ya kimaisha, maamuzi niliyoyafanya yalikuwa ni muhimu sasa kwa maslahi yangu na familia yangu.

“Nimuombe radhi aliyekuwa meneja wangu Jemedari Saidi Kazumari kutokana na sintofahamu iliyotokea kwa kutomshirikisha nikiamini asingekubali nihame mtaa.

 “Nimelazimika kufanya maamuzi magumu kwa maslahi mapana yangu mwenyewe na familia yangu.

 “Kikubwa ni kwamba Mpira ni familia moja, bado tuko kwenye familia,hakuna chuki maisha yaendelee.

“Niwashukuru wanaYanga wote kwa ushirikiano walionipatia, nilikuwa na furaha sana kwao. Pia niwashukuru viongozi wa Yanga chini ya mzee Msolla. Mimi ni mwanadamu, kiumbe dhaifu, Maana aliekamilika ni Mola wetu pekee. Nawaomba radhi sana,” amemaliza Michael.

SOMA NA HII  ZAHERA ASHUSHA KOCHA MPYA YANGA