Home Uncategorized ZAHERA ASHUSHA KOCHA MPYA YANGA

ZAHERA ASHUSHA KOCHA MPYA YANGA


KATIKA kuliboresha benchi lao la ufundi, uongozi wa Yanga upo kwenye mazungumzo ya mwisho na Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime kwa ajili ya kumletea msaidizi Mwinyi Zahera.

Hiyo, ni mara ya pili kwa Yanga kutangaza kumpa ukocha msaidizi wa timu hiyo ambaye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara atakuwepo kwenye sehemu ya benchi la ufundi. Maxime akiwa na Kagera amekuwa akiwapa ugumu Mabingwa wa ligi, Simba katika misimu hii miwili ukiwemo huu ambao imewafunga nyumbani na ugenini.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, mazungumzo yanakwenda vizuri na kama yakikamilika basi ataingia makubaliano ya miaka miwili. Mtoa taarifa huyo alisema, Zahera ndiye amevutiwa na kocha huyo kabla ya viongozi kulipitisha jina la Maxime kuwa msaidizi wake huku Mzambia, Noel Mwandila akiendelea na nafasi yake ya kocha wa viungo.

“Hatutaki masihara kwenye msimu ujao wa ligi, mengi tumepania kuyafanya na kati ya hayo ni kuhakikisha tunauchukua ubingwa wa ligi,”alidokeza mmoja wa vigogo wa Yanga. Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kwa sasa wana mambo mengi ikiwemo kuliboresha benchi la ufundi na wataweka wazi badae.

SOMA NA HII  ROLLERS: YANGA SIO WA MCHEZOMCHEZO, TUTAPAMBANA NAO KIBISHI NYUMBANI