Home Simba SC ‘GUTY’ HUYOO SIMBA

‘GUTY’ HUYOO SIMBA


INAELEZWA kuwa klabu ya soka ya Simba ipo kwenye mipango ya kumsajili kiungo mkabaji wa klabu ya Kagera Sugar, Abdulswamad Kassim ‘Guty’ ili kukiongezea nguvu kikosi hicho kuelekea msimu ujao. 

Simba inataka kuongeza ufanisi wa nafasi hiyo ya kiungo mkabaji, hasa baada ya kuwepo kwa sintofahamu ya utovu wa nidhamu wa mara kwa mara wa Jonas Mkude.

Nafasi ya kiungo mkabaji ndani ya Simba kwa sasa ina wachezaji wawili wa asili ambao ni Mzamiru Yassin, na Mganda, Taddeo Lwanga.

SOMA NA HII  KIBADENI ATAKA ONYANGO, WAWA, MORRISON NA MANULA KUTEMWA SIMBA...SABABU ZAKE HIZI HAPA....