Home Habari za michezo MAPYA YAIBUKA ROBERTINHO AFUNGUKA MAZITO BAADA YA KUTUA DAR WAKITIKEA UTURUKI, ISHU...

MAPYA YAIBUKA ROBERTINHO AFUNGUKA MAZITO BAADA YA KUTUA DAR WAKITIKEA UTURUKI, ISHU IKO HIVI

BAADA ya kikosi cha Simba SC kurejea wakitokea Uturuki, Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera (Robertinho) ameweka wazi atakuwa na wakati mgumu kupanga kikosi cha timu hiyo kutokana na wachezaji wake wamezidi kuimarika.

Amesema uimara wa wachezaji hao umetokana na maandalizi mazuri yanayoendelea kufanyika na benchi lake na kuwepo kwa wachezaji bora katika kila idara.

Baadhi ya mastaa hao waliopo kwenye kikosi hicho ni Clatous Chama, Jean Baleke, Sadio Kanoute, Saido Ntibazonkiza, Kibu Denis, John Bocco. Mohammed Hussein na Shomary Kapombe.

Mbali na hao wapya ni Luis Miquissone, Willy Essomba Onana, Kramo Aubin, Che Fondoh Malone, Fabrice Luamba Ngoma, wazawa ni Iddi Chilunda na David Kameta.

Simba walikuwa kambini Uturuki kujiandaa na msimu mpya wa 2023 /24 wa mashindano ya ndani na Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo katika maandalizi yao wamecheza mechi nne za kirafiki wakishinda mbili sare moja na kupoteza moja.

mara baada ya kuwasili nchini, Robertinho alisema timu yake imesheheni wachezaji wazuri, wale waliokuwepo msimu uliopita na wapya ambao wote wamekuwa na uwiano mzuri katika viwango vyao.

Alisema wanaenda kuyatumia makundi mawili, kundi la kwanza liko daraja la juu likiwa na wachezaji bora zaidi kuliko msimu uliopita na kila mmoja akiwa na kiwango kizuri na kuonyesha ushindani mkubwa wa kutaka namba.

“Naipongeza klabu ya Simba, Rais wa Heshima, na watendaji wengine kwa kazi waliyoifanya, kwa sababu sasa tuna uwiano mzuri wa kufanya mabadiliko ya wachezaji tunapopata majeruhi kwenye kikosi cha kwanza ni jambo la muhimu sana kuwa na kikosi kipana,” alisema Robertinho.

Aliongeza kuwa watamuheshimu kila mpinzani watakae kutana naye lakini malengo yao ni kutwaa mataji yaliyo mbele yao na kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa.

Robertinho ameeleza kuvutiwa na uwezo wa nyota wapya kwenye Kikosi akiwemo Fabrice Ngoma ambaye ameonyesha uwezo mkubwa wakiwa Uturuki, huku malengo yao kama timu ni kushinda Makombe.

Alisema anaamini kiwango cha kiungo huyo, anataka kumuona akitumia kiwango chake kutoa mchango katika timu ili wafikie malengo yao msimu ujao kimataifa.

Alisema kiungo huyo ana CV kubwa ya kuzichezea klabu kubwa Afrika, ana uzoefu wa kucheza michuano mikubwa, anataka kumuona akitumia kipaji chake kuipa mafanikio Simba msimu ujao.

“Kwa kushirikiana na wachezaji wenzake, naamini ataifanyia mengi makubwa Simba huku akitoa nafasi ya kujiandaa zaidi kwa kuongeza mazoezi ya fitinesi ili awe fiti zaidi ya hapo.

“Ngoma ni kati ya wachezaji ninaowategemea kuelekea msimu ujao, nimempa kazi kubwa ya kuhakikisha anaipambania timu kutokana na uzoefu wake wa kucheza michuano mikubwa ya kimataifa,” alisema Robertinho.

“Kwangu sina hofu kabisa, katika mchezo wa kirafiki tuliocheza Ngoma alicheza katika kiwango kikubwa, lakini hajaonyesha ubora wake ambao ninaufahamu,” alisema Robertinho.
@@@@

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Hafiz Konkoni amesema anaimani na uwezo wake na atafanya vizuri ila bado anahitaji kupata muda wa kuendelea kuzoea mazingira ya Ligi ya Tanzania.

Nyota huyo amewataka mashabiki wa Yanga kuwa na subira na kumuamini ili kuweza kusaidia timu hiyo kwa msimu mpya wa 2023/24 kwa mashindano ya ndani na kimataifa.

Konkoni aliyekuwa chaguo la pili badala ya Mcameroon, Emmanuel Dikongue, ambaye dili lake likikufa baada ya kushindana katika maslahi ambaye alitaja kuja kuchukuwa nafasi ya Mayele, aliyetimkia klabu ya Pyramids ya Misri.

Konkoni, alisema hawezi kujitabilia atafunga mabao mangapi, anachoamini ni kuwa atafanya vizuri hivyo anaomba mashabiki wawe na aimani.

Alisema atachukuwa muda mrefu kwa kuwa bado anahitaji kuelewana na wenzake pamoja na kuifahamu vizuri ligi ya Tanzania licha ya kuhakikisha hatopoteza nafasi yake ya kuitwa kwenye timu ya Taifa ya Ghana.

“Kiukweli siuwezi kutabiri kuwa nitafunga mabao mangapi, kazi yangu ni kufunga, naamini mashabiki wa Yanga watafurahi wanapaswa kuwa na imani, Sijaja kuziba pengo la Mayele, alikuwepo hapa na alifanya vizuri,” alisema nyota huyo.

Aliongeza kuwa Mayele alifanya vizuri na anauheshimu mchango wake kwenye timu hiyo, amekuja kusaidia Yanga kupata matokeo mazuri na hataku kutoa ahadi ya kufanya kama mshambuliaji aliyopita kwa kuwa hataki kucheza kwa presha.

Alisema anahitaji kupata muda wa kujiweka vizuri na kuhakikisha anapata nafasi katika kikosi cha kwanza kusaidia timu hiyo kupata matokeo mazuri katika kila mechi zilizopo mbele yao.

“Ghana kuna wachezaji wengi wazuri, kila mchezaji anapambana kuhakikisha anapata mafanikio makubwa pamoja na kuitangaza vyema nchi yetu,” alisema nyota huyo aliyecheza katika ngazi zote za timu ya taifa za vijana kuanzia U-17.

SOMA NA HII  WAMBA KAZINI HUKU REKODI SIO ZA MCHEZO