Home Uncategorized STARS YAPIGWA 2-0 AFCON NA SENEGAL

STARS YAPIGWA 2-0 AFCON NA SENEGAL


Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kimepoteza mchezo wa kwanza wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kufungwa mabao 2-0 na Senegal.

Stars imepoteza mchezo wake ikiwa ni mara ya kwanza inashiriki mashindano hayo baada ya miaka 39 kupita.

Mabao ya Senegal yamewekwa kimiani na Keita Balde mnamo dakika ya 28 na Krepin Diatta katika dakika ya 64.

Ushindi huo wa Senegal unaiweka Taifa Stars katika nafasi ya nne ya msimamo wa kundi C huku Senegal ikishika nafasi ya kwanza ikiwa na alama tatu.

Wakati huo Kenya na Algeria wanakipiga baadaye majira ya saa tano kamili za usiku.


SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR: TUTAVUNJA MWIKO WA AZAM FC KUTOFUNGWA