Home Uncategorized MWADUI WABISHI KINOMAA, WAIKOMALIA GEITA

MWADUI WABISHI KINOMAA, WAIKOMALIA GEITA

Salim Aiyee mshambuliaji wa Mwadui FC leo ameibuka shujaa baada ya kufunga mabao 2 ya ushindi yaliobakiza timu yake Ligi Kuu Bara.

Aiyee alianza kucheka na nyavu dakika ya 32 kabla ya Geita kusawazisha dakika ya 50 kupitia kwa Baraka Jerome.

Zikiwa zinahesabiwa sekunde kadhaa mchezo kuisha Aiyee aliwanyanyua mashabiki wa Mwadui FC kwa kupachika bao la pili dakika ya 90.

 Baada ya kupachika bao hilo Aiyee alivua Jezi hali iliyomlazimu mwamuzi kumuonyesha kadi ya njano.

Hivyo kwa matokeo hayo, Geita anarejea Ligi Daraja la Kwanza na Mwadui anarejea kwenye anga za TPL.

SOMA NA HII  SIMBA YAIPIGA YANGA 4G, SASA KUKUTANA NA NAMUNGO