Home Uncategorized NYOTA HAWA WATATU KIKOSI CHA KWANZA SIMBA WAMSHANGAZA MBELEGIJI

NYOTA HAWA WATATU KIKOSI CHA KWANZA SIMBA WAMSHANGAZA MBELEGIJI

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa anaona ajabu kwa nini nyota wake watatu wa kikosi cha kwanza hawajaitwa timu ya Taifa itakayoshiriki michuano ya Afcon nchini Misri mwezi Juni mwaka huu.

Aussems amesema kuwa ni muda wa Taifa kutumia wachezaji wenye uzoefu wa mashindano ya kimataifa kwa kuwa wana changamoto mpya ambazo wamezipitia.

“Kwa Taifa ambalo linaingia kwenye michuano ya kimataifa kuna haja ya kuwatumia wachezaji wale ambao wameshiriki michuano ya kimataifa, vijana kama Ndemla,(Said), Rashid (Juma) Salamba (Adam) ni miongoni mwa wenye uzoefu wa kimataifa kwa kuwa wameshiriki michuano ya kimataifa na timu imefika hatua ya robo fainali.
“Uwepo wao ndani ya kikosi ungefanya kuwe na changamoto ya namba ila maamuzi ya mwalimu huwezi kumpangia kwa kuwa naye ana mtazamo wake,” amesema Aussems.

SOMA NA HII  BAO PENDWA LA KIUNGO FUNDI WA SIMBA HILI HAPA