Home CAF KIBADENI ATAKA ONYANGO, WAWA, MORRISON NA MANULA KUTEMWA SIMBA…SABABU ZAKE HIZI HAPA….

KIBADENI ATAKA ONYANGO, WAWA, MORRISON NA MANULA KUTEMWA SIMBA…SABABU ZAKE HIZI HAPA….


Klabu ya Simba imeshauriwa kuwapa mkono wa kwaheri mabeki wake wa kigeni, Joash Onyango na Pascal Wawa ambao ni miongoni mwa wachezaji tisa wanaoelekea kumaliza mikataba yao.

Wengine ambao wametakiwa kupewa mkono wa kwaheri ni Meddie Kagere, Chris Mugalu na Bernard Morrison ambao pia mikataba inaelekea ukingoni.

Wachezaji wazawa Hassan Dilunga, Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mzamiru Yassin klabu hiyo imeshauriwa kuangalia mmoja au wawili kuwapa mikataba mipya baada ya kumaliza mikataba msimu huu.

Kocha wa zamani wa timu hiyo ambaye aliacha rekodi kadhaa enzi zake za uchezaji Simba, Abdallah Kibadeni alisema jana kwamba klabu hiyo inapaswa kufanya uamuzi mgumu kwenye kikosi.

“Kiuhalisia wachezaji wengi ambao wanamaliza mikataba yao umri ulishakuwa mkubwa. Lazima Simba ikubali kuwapa nafasi vijana kuondoa asilimia kubwa ya wale wanaomaliza mikataba yao,’ alisema Kibadeni, kocha na mshambuliaji nyota wa zamani wa timu hiyo.

“Onyango ni mchezaji mzuri, lakini hesabu za mpira ni kama zinapungua. Ndiyo sababu amekuwa akisababisha matatizo ikiwamo kucheza rafu. Morrison kuna wakati ana faida kwenye timu na kuna muda ni shida, japo kuna mechi uwa anafanya vitu vya kusaidia timu kupata matokeo mazuri, ana vitu vya ziada uwanjani na akipata nafasi ana itumia, ingawa shida iko kwenye nidhamu yake,” alisema kocha huyo.

Ali-sema kwa Manula bado kiwango chake kiko vizuri japo umri umesogea, lakini hana shaka akipewa nafasi nyingine Simba atacheza kwa kiwango chake.

“Kuna haja ya Simba kuwabakisha wakongwe wachache katika timu ili kuwasaidia akiwamo Manula, ingawa kwa Nyoni pia ni kama umri umesogea na wakati mwingine kisoka kupata majeraha ya mara kwa mara inatokea.”

Alisema Dilunga haonyeshi makeke kama ilivyokuwa awali anacheza kwa uhakika tangu alipokuwa naye JKT anaufahamu uwezo wake, ingawa kwa sasa amepunguza makeke uwanjani.

“Mzamiru pia japo anacheza kwa uhakika, lakini kama nilivyosema kuna mahali nguvu zinapungua, hivyo Simba wanahitaji kukifanyia maboresho kikosi chao na kuwapa fursa zaidi vijana.”

SOMA NA HII  BARBARA APIGA STOP USAJILI MPYA SIMBA...ADAI WALIOIPIGANIA TIMU WATAPEWA KIPAUMBELE....

Alisema eneo la ushambuliaji timu hiyo inahitaji kuboresha zaidi, japo kuna Kagere na John Bocco ambao kutokana na zoefu wao wana faida, lakini haipaswi kuwa na wachezaji wenye umri mkubwa wengi.

“Wakiwa na wachezaji wa aina hiyo mmoja au wawili wanatosha ambao watakuwa benchi wakisubiri vijana wapambane, wakishindwa ndipo wanaingia wao kuokoa jahazi au kinyume chake,” alisema.

Hata hivyo, mwenyekiti wa bodi ya klabu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ alifichua kuanza mazungumzo na baadhi ya wachezaji wao ambao mikataba yao inaelekea ukingoni akiwamo Manula.

Meneja wa kipa huyo, Jemedari Said aliliambia gazeti hili mazungumzo ya kumuongezea mkataba mpya yako katika hatua nzuri na kwa asilimia kubwa huenda akabaki Simba baada ya kumaliza mkataba wake.