Home Habari za michezo KISA MEYELE KUSEMWA VIBAYA…MANARA ACHARUKA…ATUPA DONGO AZAM NA KWA MSEMAJE WAO….

KISA MEYELE KUSEMWA VIBAYA…MANARA ACHARUKA…ATUPA DONGO AZAM NA KWA MSEMAJE WAO….


Baada ya kuzungumza katika mahojiano na Vyombo vya Habari kabla ya mchezo wao dhidi ya Yanga, Afisa Habari wa Azam FC, Thabiti Zakaria “zakazakazi” kuhusu ubora wa Mayele.

Zakazakazi anadai kuwa Mayele ni mchezaji wa kawaida tu, na kuthibitisha hilo alikwenda mbali na kutoa takwimu za wafungaji katika ligi Kuu Bara tangu mwaka 1996 akionesha idadi ya magoli ambayo washambuliaji walifunga.

Sasa msemaji wa Yanga, Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuhusiana na ubora wa Mayele na kutoa maneno ambayo yanaonekana kama dongo kwa Zakazakazi.

Manara ameandika;

“Licha ya kuzibandua team kibao nchini lakini This Guy ni Gentleman sana, ni mtu mtaratibu mno nje ya Uwanja, kisha ni Mkatoliki halisi anaesali St Peter’s pale Osterbay, very popular pale kanisani kwake kama ilivyo mtaani.

Hebu isome hii picha na jinsi battle yao ilivyokuwa na @agreymorisambros, kisha sikia alichokisema baada ya mechi kuhusu ubora wa Agrey.

Fikiria teke alilipigwa jana na Yondan bila sababu, ingekuwa hawa Washambuliaji wetu zingelika ngumi pale.

Najua kuna wengine wana wivu na choyo dhidi yake, lakini lini watu wa aina hiyo wataisha duniani?

Wananchi wenzangu, hebu waulizeni kwanza, hao washambuliaji wa miaka ya themanini waliosema eti waliwaona wakicheza,,waliwaonea wakiwa wapi? Kwao Nyampipi kulikuwa na team ya ligi kuu hadi awaone? Tv zilikuwepo? Labda hawa wa kuanzia 2000 kina Shengo Tondolo na Abdallah Juma pamoja na Henri Morris.

Zamoyoni Mogella, Peter Tino, Mohammed Salim, Ally Katolila, Makumbi Juma, Innocent Haule, Juma Mgunda, Saidi Mrisho, Kitwana Suleiman…

hao ni miongoni mwa Strikers wakubwa wa miaka ya themanini, uliwaona ukiwa wapi? Au Ahmed Jongo na Dominic Chilambo pamoja na Ahmed kipozi walikusimulia through Radio Tanzania?

Acha tunyamaze tu ila @mayelefiston kaishika hii nchi, choyo hazimzuii kuendelea kuwapakata, Yes Naitwa Haji Fiston Sunday Kalala Bugati Pele Manara wa Mayele, ukinuna natuma goli la Juzi”

SOMA NA HII  TETESI:- MKUDE NA YANGA MAMBO NI BULBULI...SKUDU MAPEMA TU 'KALAMBA SHAVU' JIPYA...