Home Habari za michezo TIZI LA YANGA SIO POA KAMA ULAYA UNAAMBIWA

TIZI LA YANGA SIO POA KAMA ULAYA UNAAMBIWA

Habari za Yanga

KATIKA kuhakikisha Yanga inazidi kufanya vema katika mchezo unaofuata wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merrikh, benchi la ufundi la timu hiyo likiongozwa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, limeanza kuwafungia wachezaji vifaa maalum vya kupima ufanyaji wao mazoezi.

Hiyo imekuwa ikionekana kwa wachezaji wengi wa Ulaya ambao mara nyingi hutumia vifaa hivyo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa hawategei uwanjani.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habri wa Yanga, Ally Kamwe, alisema sababu kubwa ya Kocha Gamondi kufanya hivyo ni kuhakikisha wachezaji hawategei program za mazoezi kwani wanapomaliza huwachuguza kwa kuangalia vifaa hivyo.

“Mwalimu hataki kuona wachezaji wanategea uwanjani, ndio maana wameamua kuwafungia vifaa maalum vya GPS kwa ajili ya kuwachunguza wachezaji wote wale ambao wanategea kufanya mazoezi.

“Vifaa hivi kama mchezaji utategea basi lazima itajulikana kwa kuwa baadaye huvisoma kwa kila mchezaji na kufahamu ambaye hakufanya mazoezi kwa kujituma, kocha anataka wachezaji wote wawe timamu tayari kwa ajili ya mapambano ya dakika 90 na wala sio kuchoka mapema,” alisema Kamwe.

SOMA NA HII  FT: YANGA 5-0 ZALAN FC .....MAYELE ATETEMA KWA HASIRA....AZIZ KI ATOA GUNDU TENA...GEITA GOLD SAWA LAKINI HAITOSHI..