Home Habari za michezo BAADA YA KUSAJILIWA NA KUTOONEKANA…YANGA WAIBUKA NA KUANIKA ALIPO BEKI WAO MPYA..

BAADA YA KUSAJILIWA NA KUTOONEKANA…YANGA WAIBUKA NA KUANIKA ALIPO BEKI WAO MPYA..

Habari za Yanga

Kijana mwenye maneno yake 10 enzi hiyo kabla hajawa Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe, ameweka wazi ni wapi alipo Beki la CHAN Mamadou Doumbia kutoka Mali, na kwanini hakucheza mchezo dhidi ya Monastir licha ya kuambiwa ni beki mwenye kiwango kikubwa.

Kamwe alisema kuwa kwenye mechi iliyopita hakuwa kwenye mipango ya Kocha Nasradinne Nabi, lakini pia alifafanua sababu zinazomfanya kutocheza na Yanga mpaka sasa tangu atue Avic Town kwenye kambi ya Yanga.

“Doumbia alikosekana kwenye mchezo uliopita kutokana na kutokuwa kwenye mipango ya mwalimu”-Ali Kamwe.

“Doumbia ni ingizo jipya la dirisha dogo, mashabiki wanapaswa kuelewa kuwa mchezaji huyo anahitaji muda ya kucheza na wenzake kutokana na eneo lake la uchezaji kuwa na umuhimu mkubwa zaidi, ni mchezaji mzuri mwenye kiwango kikubwa lakini kucheza na Job, Mwamnyeto na Bangala anahitaji kuzoeana nao, bado anafanyia kazi muunganiko na wenzake”

Kwa Upande wa Kocha Mkuu wa Yanga Nasradinne Nabi alielezea namna ambavyo anamuandaa Beki huyo kuwa fiti sana.

“Watu wanaongelea sana kuhusu Doumbia, sio kila mchezaji akiletwa basi ataanza kucheza, huyu ni beki wa kati hili ni eneo ambalo unahitaji utulivu kumuingiza, tunafanya kazi kubwa sasa ya kumfanya anazoea.”-Nabi

SOMA NA HII  KUELEKA MECHI NA DODOMA JIJI KESHO....GAMONDI KUSHUKA NA GIA ZOTE ZA CAF