Home Habari za michezo WAKATI WENZAKE WAKIWA ‘BUSY’ NA MECHI YA KESHO…MORRISON AJIPA JINA LA ‘MR...

WAKATI WENZAKE WAKIWA ‘BUSY’ NA MECHI YA KESHO…MORRISON AJIPA JINA LA ‘MR PANYA’ ….

Habari za Yanga

Nyota wa kikosi cha Yanga, Bernard Morrison raia wa Ghana ameamua kubadili muonekano wake na kuweka muonekano mpya baada ya kunyoa nywele zote kichwani na kuziachia ndevu.

Morrison ambaye amekuwa haishiwi vituko tangu aje Tanzania mwaka 2019, amesema aitwe ‘Mr. Panya. “I know I now look like a mouse so don’t even bother yourself to tell me. Just call me Mr Panya????”

Morrison tangu arejee Yanga msimu huu kwenye ligi kuu ametumika katika mechi 10 akiyeyusha dakika 450, amefanikiwa kifunga mabao 2 na ana asisti 2 tofauti na yalivyokuwa matarajio ya Yanga wakati wakimsajili.

Winga huyo kwa sasa ameachwa kujumuishwa katika kikosi cha timu hiyo kinachoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa kile kilichoelezwa kuwa ana majeraha ya groin.

Morrison ambaye mara ya mwisho kuitumikia Yanga ilikuwa mechi waliyoshinda mabao 3-2 dhidi ya Azam Desemba 25, mwaka jana alielezwa kuwa yuko kwao Ghana kwa ruhusa kabla ya baadaye kuelezwa ana majeraha hayo.

Rais wa klabu hiyo, Hersi Said alikaririwa akisema ingawa hakuwa na majeraha ya kumuweka nje moja kwa moja lakini imewalazimu kumuacha ili apone kabisa na aisaidie timu katika kipindi kigumu cha mwisho wa msimu.

Yanga itashuka Dimbani kesho Jumapili, Februari 19, kuvaana na TP Mazembe ya Congo katika mchezo wao wa piliu wa Kundi D katika kombe hilo la Shirikisho Afrika utakaopigwa katika Dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 1:00 jioni.

SOMA NA HII  YACOUBA NA KAMBOLE WITWA RASMI YANGA...KISINDA, MAKAMBO NA BIGIRIMANA KUWAPISHA ...