Home Habari za michezo YACOUBA NA KAMBOLE WITWA RASMI YANGA…KISINDA, MAKAMBO NA BIGIRIMANA KUWAPISHA …

YACOUBA NA KAMBOLE WITWA RASMI YANGA…KISINDA, MAKAMBO NA BIGIRIMANA KUWAPISHA …

Dirisha dogo la usajili linafunguliwa wiki ijayo. Yanga imewapigia simu mastraika wawili, Lazarous Kambole na Yacouba Sogne warejee kikosini haraka ili wawaangalie kabla ya kufanya uamuzi.

Yanga inaoongoza msimamo kwa sasa ikiwa na pointi 32 baada ya mechi 13, itashuka uwanjani keshokutwa kuvaana na maafande wa Tanzania Prisons, lakini mabosi wa timu hiyo wanawaza kuboresha safu ya ushambuliaji kwa ajili ya michuano ya ndani na ile ya Shirikisho.

Huku ikisubiri droo itakayofanyika Desemba 12, katika kusuka safu hiyo ya ushambuliaji inataka kuanza na mastraika hao, wakiangalia uimara wao kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho kuwaingiza kikosini kupitia dirisha dogo la usajili kuungana na Fiston Mayele, Stephane Aziz KI pamoja na Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Taarifa kutoka ndani ya mabosi wa Yanga ni kwamba kocha Nasreddine Nabi anataka mechi mbili za kirafiki zitakazotumika kuwapima washambuliaji hao waliochomolewaga kwa nyakati tofauti.

“Yacouba alishapona na alikuwa anafanya mazoezi makali, lakini tunataka tumuone anapocheza mechi ana utayari kwa namna gani, sote tunamjua, ilani vyema tukajiridhisha zaidi,” alisema mmoja wa mabosi wa klabu hiyo,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Kambole naye tutamwangalia kama kwa sasa ni mtu muafaka kuja kutuongezea kitu na kocha (Nasreddine Nabi) atafanya maamuzi na wasaidizi wake.”

Ujio wa washambuliaji hao huenda ikaongeza presha kwa baadhi ya mastaa wa kigeni katika kikosi hicho ambapo kama watapitishwa wote wawili,uhakika kuna vichwa viwili vitalizimika kupisha.

Yanga tayari ilishakamilisha idadi ya kikanuni ya wachezaji wa kigeni wakiwa na watu 12 ambapo maamuzi ya kuwaingiza wengine watalazimika kupunguza wengine.

Kambole jina lake lilienguliwa mwishoni mwa dirisha kubwa lililopopita ili kumpisha Tuisila Kisinda ambaye hata hivyo ameshindwa kung’ara tofauti na ilivyotarajiwa na anatajwa ni kati ya wachezaji wanaoweza kupigwa chini ili kuwapisha kina Yacouba.

Wengine waliopo kwenye hatihati ya kupigwa panga ni Heritier Makambo na Gael Bigirimana, kwani kwa mujibu wa kanuni ya usajili wa wageni kwa kila klabu ni wachezaji 12, idadi iliyonayo kwa sasa.

Yanga imepania kufanya makubwa kwenye michuano ya kimataifa na kurejesha hadhi yake iliyochuja kwa miaka kadhaa. Kocha Nabi alisema hivikaribuni kwamba lazima afanye usajili wa maana kuongeza nguvu kikosini licha haswa kwenye safu ya kiungo, ushambuliaji na ulinzi licha ya kwamba kwenye jicho la kishabiki timu imeonekana ikifanya vizuri kwenye Ligi ya ndani.

SOMA NA HII  YANGA WAPEWA MBINU YA KUPINDUA MEZA KIBABE LEO KIMATAIFA