Home Habari za michezo WAKATI TANZANIA WAKIIBEZA ‘UNBEATEN’ YA YANGA….LA LIGA NA CAF WAITOLEA MFANO KWA...

WAKATI TANZANIA WAKIIBEZA ‘UNBEATEN’ YA YANGA….LA LIGA NA CAF WAITOLEA MFANO KWA TIMU NYINGINE…

Ligi Kuu ya Hispania(LaLiga) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika(CAF) zimeipongeza klabu ya Yanga kwa kuweka rekodi ya kutofungwa michezo 49 ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Taarifa ya Laliga imesema ligi hiyo inatoa pongezi za dhati kwa Yanga kwa kuwa klabu ya kwanza Tanzania kufikia rekodi hiyo.

“Hii ni rekodi pekee Tanzania na ukanda wa Afrika mashariki na Kati,” imesema LaLiga.

Nayo CAF imesema Yanga imeandika historia katika soka la Afrika kwa kuwa miongoni mwa timu tano barani humo kuwa na rekodi ndefu ya kutofungwa katika ligi.

ASEC Mimosas ya Ivory Coast inashikilia rekodi Afrika ya kutofungwa michezo 108 wakati Esperance de Tunis ya Tunisia ni ya pili michezo 85 huku APR ya Rwanda ikiwa ya tatu kwa michezo 50.

Yanga ni ya nne wakati miamba ya soka Afrika Al Ahly ya Misri ni ya tano ikiwa na rekodi ya kutofungwa mechi 46.

Yanga imepoteza mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Novemba 29 hivyo kufikia tamati ya kutofungwa.

SOMA NA HII  MASTAA YANGA WACHOTA SH 265...GSM WAAMUA...SIMBA WAIVIMBIA..JEURI YAO HII HAPA...