Home Yanga SC YANGA WATAJA SABABU YA MWAMNYETO, NTIBANZOKIZA KUANZIA BENCHI

YANGA WATAJA SABABU YA MWAMNYETO, NTIBANZOKIZA KUANZIA BENCHI

 WAKATI timu ya Yanga ikishinda bao 1-0 dhidi ya Biashara United, nahodha msaidizi wa Yanga, Bakari Mwamnyeto na kiungo mkongwe Haruna Niyonzima walikuwa wakisugua benchi.

Ingizo jipya ndani ya kikosi hicho, beki wa kati Dickson Job alianza kwa mara ya kwanza kuitumikia timu yake hiyo, akicheza kwa dakika 90 sambamba na Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

Pia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Gwambina FC, wakati ubao ukisoma Yanga 3-1 Gwambina, Mwamnyeto, Niyonzima, Said Ntibanzokiza waliaanzia benchi.

Kwenye mchezo huo Mwamnyeto aliingia baada ya Job kuumia na Said aliingia baada ya Tuisila kuumia na nyota wote hao wawili kila mmoja alitupia bao mojamoja na kufanya timu isepe na pointi tatu mazima.

Akizungumza kuhusu wachezaji wake kuanzia benchi na kumuanzisha Job, Juma Mwambusi, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hakuna mwenye uhakika wa namba ndani ya kikosi hicho kwa sasa.

“Niliweka wazi tangu awali kwamba hakuna mwenye namba ya kudumu katika kikosi hiki. Yule ambaye atafanya vizuri kwenye mazoezi huyo anaanza kikosi cha kwanza.

“Kila mmoja ninampa nafasi ya kufanya vizuri ndio maana unaona kwamba nilianza na Ninja, kisha mechi hii ameingia Job (Dickson) hivyo bado kutakuwa na mabadiliko kwenye mechi zetu zijazo,” amesema Mwambusi.

Kwa sasa Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 57 mchezo wake ujao ni dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Jumapili, Uwanja wa Mkapa saa 2:15 usiku.


SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZANA NA YANGA..HIVI NDIVYO SURE BOY ATAKAVYOMPA WAKATI MGUMU NABI..