Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA RAJA CASABLANCA LEO…MBRAZILI SIMBA KAWAPA MBINU HII MPYA MASHABIKI..

KUELEKEA MECHI NA RAJA CASABLANCA LEO…MBRAZILI SIMBA KAWAPA MBINU HII MPYA MASHABIKI..

Habari za Simba SC

Baada ya Simba kurejea kutoka Guinea alifajiri ya jana, kocha mkuu Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema akili zao kwa sasa ni mchezo wa leo dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco, lakini akawataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kuongeza mzuka.

“Tuna kila sababu ya kupata pointi tatu kwa sababu tupo nyumbani. Mashabiki waje uwanjani kutushangilia watatupa morali na watafurahi,” alisema Robertinho.

Katika hatua nyingine mtendaji mkuu wa Simba, Iman Kajula alisema maandalizi dhidi ya Raja yalianza mapema kwa sababu Simba ni taasisi na miongoni mwao walibaki nchini kuendelea na taratibu zingine.

Kajula alisema maandalizi yamekamilika na wanawaheshimu wapinzani wao kwa sababu wanajua wapo kwenye kundi lenye timu ngumu kama ilivyo wao wenyewe.

“Tupo kundi gumu na tunatakiwa kuwaheshimu wapinzani wetu kwa sababu wote ni timu ngumu na sisi ni mojawapo. Simba ni timu kubwa na ndio maana wachezaji wanacheza kwa hali ya juu,” alisema.

“Upande wa bonasi sitaki kuzungumzia kwa sababu tutaweka presha kwa familia na wachezaji lakini mtambue Simba ni timu kubwa na huwa inafanya vitu vyake kimya kimya.”

Mshambuliaji wa timu hiyo Jean Baleke akizungumzia mchezo dhidi ya Raja alisema watapambana kuhakikisha wanabakiza pointi tatu nyumbani.

“Raja ni timu kama ilivyo Simba na mchezo utakuwa mzuri kwa timu zote mbili. Kucheza kwetu nyumbani tunahitaji pointi tatu na sio kitu kingine,” alisema. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa 1:00 uziku katika Uwanja wa Mkapa ambapo mchezo wa kwanza dhidi ya Horoya ya Guinea, Simba ilifungwa bao 1-0.

SOMA NA HII  MZIZE AFUNGUKA A-Z KUHUSU UTAMU WA KUANZIA BENCHI YANGA NA KUNAVYOMPA MAAJABU..