Home news SIKU CHACHE BAADA YA KUPIGWA CHINI KUTENGENEZA JEZI ZA SIMBA…VUNJA BEI AIBUKA...

SIKU CHACHE BAADA YA KUPIGWA CHINI KUTENGENEZA JEZI ZA SIMBA…VUNJA BEI AIBUKA NA KUANIKA HAYA…

Habari za Simba leo

Mkurungezi wa Kampuni ya Vunjabei Fred Ngajilo ametoa Shukrani kwa Klabu ya Simba Sports Club kwa kumuamini na kufanya nae kazi kwa Miaka Miwili huku akisema kuwa wameleta mapinduzi makubwa kwa Tasnia ya Utengenezaji na usambazaji wa Jezi na vifaa vya Michezo, Kupitia ukurasa wake wa Instagram #Fred ameandika….

“Verified Menejimenti ya Vunjabei (T) Group Limited inapenda kutoa shukrani za dhati kwa bodi ya wakurugenzi, menejimenti, benchi la ufundi, wachezaji, wanachama na mashabiki wote wa Simba Sports Club kwa ushirikiano mkubwa ambao wamekuwa wakitupa katika kipindi chote cha miaka miwili ambayo tumefanya kazi ya Mapinduzi makubwa ya tasnia hii ya utengenezaji na usambazaji wa vifaa vya michezo.

Tunatarajia kuendelea kudumisha uhusiano huu tulioujenga, tunachukua fursa hii kumpongeza mzabuni mpya na hatutasita kumpa ushirikiano wa aina yeyote pale tutakapohitajika.

Tunaamini kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kuelekea kwenye mafanikio zaidi na kusababisha maendeleo katika mpira wetu wa miguu Tanzania.

SOMA NA HII  SAA CHACHE KABLA YA DABI...MKWASA ASHINDWA KUJIZUIA..AANIKA TIMU ITAKAYOFUNGWA LEO..AITAJA YANGA..