Home news KISA KIWANGO CHA MOLOKO…BAHANUZI AIBUKA NA HILI ..ADAI SIO MAKINI..CHAMBUA NAYE AMLIPUA..

KISA KIWANGO CHA MOLOKO…BAHANUZI AIBUKA NA HILI ..ADAI SIO MAKINI..CHAMBUA NAYE AMLIPUA..

 


WINGA wa Yanga, Jesus Moloko kwa kasi aliyonayo ameshauriwa kuongeza maarifa kwenye umaliziaji jambo litakalompa urahisi wa kufanya makubwa Ligi Kuu Bara.

Tangu amejiunga na Yanga msimu huu, Moloko amecheza mechi 13 za ligi na hajacheza dakika 90, huku akicheza dakika chache zaidi (23) dhidi ya Tanzania Prisons, ambapo dakika alizocheza katika mechi 13 ni 886, jambo ambalo wadau wameona kitu cha ziada kwake. wadau walidai Moloko ana vitu miguuni ambavyo hajavionyesha na kumtaka aongeze bidii ili atishe.

Staa wa zamani wa timu hiyo, Sekilojo Chambua alisema nyota huyo ana kasi nzuri, isipokuwa anapaswa kuongeza maarifa katika umaliziaji wa mipira ya mwisho.

“Ana kasi nzuri inayoendana na nafasi anayocheza. Pamoja na hilo siyo mzuri kwenye umaliziaji wa mipira ya mwisho, ila akiongeza bidii katika hilo ataifanyia mambo makubwa Yanga,” alisema.

Straika wa zamani wa timu hiyo, Said Bahanuzi alisema kwa mbio zake akiwa na umaliziaji mzuri anaweza kufunga mabao na kutoa asisti nyingi. “Ana kasi ambayo inaweza kuwa mwiba kwa mabeki, isipokuwa aongeze umakini kwenye kumalizia mipira ya mwisho.”

Kipa wa zamani wa Simba na Yanga, Steven Nemes alisema Moloko anapaswa kuboresha umaliziaji ili kuendana na kasi yake.

SOMA NA HII  VITENDO VYA RONALDO BAADA YA MAN UTD KUFUNGWA 4-0 KUMFUKUZISHA OLD TRAFORD...AC MILAN WAJIANDAA KUMCHUKUA...