Home Habari za michezo KOCHA WA TAIFA STARS ATEMA ‘CHECHE’ SAKATA LA MSUVA NA TIMU YAKE…AMPA...

KOCHA WA TAIFA STARS ATEMA ‘CHECHE’ SAKATA LA MSUVA NA TIMU YAKE…AMPA SHARTI ZITO..LA SIVYO …


KOCHA wa timu ya Taifa Tanzania, Kim Poulsen amemtaka mchezaji wake Simon Msuva kumaliza utata wake na klabu yake ya Wydad Casablanca ili arejee uwanjani.

Msuva yupo nje ya uwanja baada ya kuwa na mvutano na klabu yake hali iliyomfanya arudi nchini na kuendelea kujifua kivyake.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kumita mchezaji huyo kwenye kikosi chake, Poulsen alisema anafahamu Msuva yupo nchini na mara kwa mara anazungumza nae kuona namna gani anamsaidia.

“Mara kwa mara huwa nazungumza nae na nimemuambia kabisa ahakilishe anamaliza suala lake na timu yake kwa sababu anatakiwa acheze kwa haraka” alisema Kim.

Akizungumzia kuhusu kumrejesha kikosini kinda Kelvin John alisema amelizika na kiwango ambacho amekionyesha mchezaji huyo.

Kim alisema yeye binafsi pamoja na watu wake wengine wamekuwa wakimfatilia mchezaji huyo nw kuona anafaa kurejea kwenye kikosi chake.

“Awali alikuwa yupo shule akawa anacheza na alipoenda Ubeligiji nilimtuma mtu akawa anamfuatilia kwa ukaribu na kunipa ripoti zake, mimi na kocha wa KRC Genk bahati nzuri ni marafiki kwahiyo napata Catapult (kipimo cha mikimbio) na nimeona anafaa,” alisema Kim.

Akizungumzia kuhusu wachezaji wake wapya kwenye kikosi alisema ni jambo la kawaida kuweka sura mpya na anaamini hazitomuangusha.

“Hata wakati namuita Novatus (Dismas) kila mmoja alikuwa anasema lake lakini mwisho wa siku alionyesha kitu kikubwa kwahiyo hata hawa naamini wataonyesha kitu,” alisema Kim na kuongeza;

“Pia kwenye mechi mbili za kirafiki ambazo tutacheza nitapata taswira nzima ya wachezaji ambao nimewaita.”

SOMA NA HII  UNAHANGAIKA KUPATA USHINDI KUPITIA CASINO....SLOT HII NI MKOMBOZI WA KWELI...