Home Habari za michezo SIMBA WATAMBA KUKUTANA NA AL AHLY, DAWA YAO HII HAPA

SIMBA WATAMBA KUKUTANA NA AL AHLY, DAWA YAO HII HAPA

Habari za Simba leo

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), Jumamosi lilichezesha droo ya michuano ya African Football League ambapo wawakilishi wa Tanzania, Simba wanatarajiwa kupambana na Al Ahly, huku wenyewe wakitamba kwa kusema: “Waje tu, tuna dawa yao kwa Mkapa.”

Michuano hiyo inayohusisha timu nane ikiwa inafanyika kwa mara ya kwanza, itachezwa kwa mtindo wa mtoano nyumbani na ugenini, huku ikitarajiwa kuzinduliwa rasmi Oktoba 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar kwa kuchezwa mechi ya robo fainali ya kwanza kati ya Simba dhidi ya Al Ahly, timu hizo zitarudiana Novemba 24. Michuano hiyo tamati yake ni Novemba 11, 2023.

Wakati robo fainali ya kwanza ikiwa ni Simba dhidi ya Al Ahly, robo fainali ya pili TP Mazembe dhidi ya Espérance. Robo fainali ya tatu ni Enyimba dhidi ya Wydad Athletic Club, huku robo fainali ya nne ni Atlético Petróleos de Luanda vs Mamelod Sundowns.

Baada ya mechi hizo za mtoano kumalizika, nusu fainali ya kwanza inatarajiwa kuzikutanisha mshindi kati ya Simba na Al Ahly dhidi ya mshindi kati ya Atlético Petróleos de Luanda na Mamelod Sundowns. Nusu fainali ya pili ni mshindi kati ya Enyimba na Wydad dhidi ya TP Mazembe na Espérance.

Mechi hizo za nusu fainali, mkondo wa kwanza utakuwa Oktoba 29, kisha marudiano ni Novemba 1, huku fainali ya kwanza ikitarajiwa kuwa Novemba 5, marudiano Novemba 11, 2023. Mechi zote zitachezwa nyumbani na ugenini hadi fainali.

Ikumbukwe kwamba, bingwa wa michuano hiyo anatarajiwa kuondoka na zaidi ya Dola za Marekani milioni 11.6 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 29 za Tanzania.

Akizungumzia droo hiyo, Meneja wa Habari wa Simba, Ahmed Ally, amesema: “Hakukuwa na sababu ya kuikwepa timu yoyote, tulijiandaa, hivyo tunajua namna ya kukabiliana na Al Ahly,waje tu.

“Michuano hii lazima ukutane na wababe wenzio ili ufikie malengo ya kuwa bingwa, hivyo tupo tayari.”

SOMA NA HII  KAPOMBE ATULIZA MZUKA SIMBA...AFUNGUKA WALICHOFANYIWA NA BENCHIKHA....