Home Azam FC DUBE APEWA TUZO YA UFUNGAJI BORA BONGO

DUBE APEWA TUZO YA UFUNGAJI BORA BONGO


 PRINCE Dube ambaye ni kinara wa mabao ndani ya ligi akiwa na mabao 12 na pasi tano za mabao anapewa nafasi ya kutwaa tuzo hiyo iliyo mikononi mwa mchezaji wa Simba, Meddie Kagere.

Kagere alitupia jumla ya mabao 22 msimu uliopita na msimu huu nyota huyo ametupia mabao 11 akiachwa kwa bao moja na Dube wa Azam FC.

Vivier Bahati, kocha msaidizi wa Azam FC amesema kuwa anaona kwamba mchezaji huyo ana nafasi ya kuweza kutwaa tuzo ya ufungaji bora kwa kuwa amekuwa na kasi pamoja na spidi katika utendaji wa kazi.

Bahati amesema:”Bado kuna mechi ambazo zipo na imani yetu ni kuona kwamba Dube anaendelea kufunga pale anapopata nafasi kwa kufanya hivyo itasaidia kuweza kutimiza malengo yake pamoja na kutimiza majukumu yake,”amesema.

Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 54. 

SOMA NA HII  AZAM FC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA JKT TANZANIA