Home FA Cup DROO YA KOMBE LA SHIRIKISHO KUCHEZWA KESHO,

DROO YA KOMBE LA SHIRIKISHO KUCHEZWA KESHO,


 DROO ya Fainali ya Azam Sports Federation Cup inatarajiwa kufanyika kesho majira ya saa 5:00 asubuhi na itaruka mubashara Azam Sports1 HD.

Mabingwa watetezi wa taji hilo ni Simba na wametinga hatua ya robo fainali baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Mkapa.

Hizi hapa ambazo zimetinga hatua ya robo fainali na zinasubiri kuona zitapangiwa na nani droo ya kesho:-

Rhino Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Biashara United, Azam FC, Mwadui FC, Yanga SC, Dodoma Jiji, Simba SC na Namungo FC. 


SOMA NA HII  BUKU KUMI TU KIINGILIO SIMBA V YANGA, MWISHO WA RELI KIGOMA