Home epl KANE AWAOMBA MABOSI WAPOKEE OFA

KANE AWAOMBA MABOSI WAPOKEE OFA


HARRY Kane, mshambuliaji wa kikosi cha Tottenham amemwambia mmiliki wa timu hiyo Daniel Levy apokee ofa ambazo zimekuwa zikimuhitaji.

Klabu mbalimbali zimekuwa zikikihitaji saini ya nyota huyo ili ziweze kupata huduma yake kwa ajili ya kuzitumikia kwa msimu ujao.

Miongoni mwa timu ambazo zimepeleka ofa ya kumpata nyota huyo ni pamoja na Manchester United ambayo iliweka dau la pauni milioni 90 kwa ajili ya kumpata mshambuliaji huyo.

Imekuwa ikieelezwa kuwa Kane amewaambia mabosi wake kwamba anataka kuondoka ndani ya Spurs ili kwenda kujiunga kwenye timu inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kichapo cha mabao 3-1 walichokipata Spurs na Leeds juzi kimepunguza matumaini kwa timu hiyo kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao na alijiunga na timu hiyo mwaka 2004.

SOMA NA HII  ZILE TETESI ZA 'BEKI KISIKI' NATHAN IDUMBA KUTAKIWA SIMBA ZIMEMUIBUA WAKALA WAKE...KAANIKA UKWELI HUU ..