Home Yanga SC YANGA WATIA TIMU KIGOMA MAPEMA KUIWAHI SIMBA

YANGA WATIA TIMU KIGOMA MAPEMA KUIWAHI SIMBA

 


KIKOSI cha Yanga leo Julai 22 kimewasili Kigoma kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Kombe la Shirikisho. 

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Lake Tanganyika,  itakuwa ni Julai 25, saa 10:00 jioni.

Wanakutana na mtani wao wa jadi Simba ambao ni mabingwa watetezi wa taji hilo ambalo walitwaa msimu uliopita mbele ya Namungo. 

Unatarajiwa kuwa mchezo mgumu kwa pande zote mbili kwa sababu wanakutana wakiwa wametoka kunyooshana kwenye ligi.

Julai 3, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga hivyo Yanga watataka kuendelea pale walipoishia kwenye ligi na Simba wakihitaji kulipa kisasi.

SOMA NA HII  NYOTA SABA WA YANGA HATIHATI KUUKOSA MCHEZO WA KOMBE LA SHIRIKISHO