Home Simba SC CHUKI ZA BARBRA ZAMPA HOFU HAJI MANARA

CHUKI ZA BARBRA ZAMPA HOFU HAJI MANARA

 HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa anahofia kula chakula akiwa mbele ya Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez kutokana na kile anachodai ni chuki kali aliyonayo kiongozi huyo.

Kupitia sauti ambayo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao sauti ya mtu anayesadikika kuwa ni Manara imesikika ikisema kwamba miongoni mwa vitu ambavyo vinampa shida ndani ya Simba ni roho ya chuki.

“Barbra wewe una chuki na roho mbaya sijawahi kuona mpaka naogopa kula chakula mbele yako. Umekuwa ukiwadhalilisha wafanyakazi wa Simba jambo ambalo ni baya,” ilisikika sauti hiyo.

Pia habari zinaeleza kuwa Manara anampango wa kubwaga manyanga Simba mara baada ya fainali Kigoma Julai 25 ambapo itakuwa ni Yanga v Simba, Uwanja wa Lake Tanganyika,  Kombe la Shirikisho.

SOMA NA HII  STAA HUYU WA SIMBA ANAJUTA KUONDOKA YANGA, STORI KAMILI IKO HIVI