Home Uncategorized NDANDA V MBAO LEO HAPATOSHI NANGWANDA

NDANDA V MBAO LEO HAPATOSHI NANGWANDA

LEO Uwanja wa Nangwanda Sijaona kutakuwa na mchezo wa kukata na shoka kati ya Ndanda FC dhidi ya Mbao FC ya Mwanza.

Mechi ya leo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na vita ya nafasi ndani ya ligi.

Mbao FC iliyo chini ya Hemed Morroc ipo nafasi ya 15 ikiwa imecheza jumla ya mechi 17 na imeshinda mechi nne, sare sita na kupoteza mechi saba huku Ndanda FC ikiwa nafasi ya 19 na pointi zake 12.

Kwenye mechi hizo 17 ilizocheza imeshinda mechi mbili na sare nne huku ikipoteza mechi 12.

Kwenye dirisha dogo la usajili, Ndanda imemrudisha mchezaji wao Vitalis Mayanga aliyekuwa anakipiga ndani ya KMC na tayari ameanza kuonesha makeke yake kwa kufunga bao moja mbele ya Alliance FC.

Mayanga amesema kuwa ushindani ni mkubwa na kila timu inapambana kutafuta ushindi.

Mbao wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kuchapwa mbele ya Namungo FC mabao 3-0.

SOMA NA HII  TWENDENI TAIFA TUKAWAPIGE PAMOJA BURUNDI TWENDE KOMBE LA DUNIA