Home FA Cup BUKU KUMI TU KIINGILIO SIMBA V YANGA, MWISHO WA RELI KIGOMA

BUKU KUMI TU KIINGILIO SIMBA V YANGA, MWISHO WA RELI KIGOMA


KUELEKEA kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba v Yanga tayari mashabiki washajua viingilio kwenye mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Ni 10, 000, (buku kumi) kwa mzunguko huku eneo ambalo limepewa jina la Urusi kiingilio chao pale ni 15,000, (buku kumi na tano).

Kwa upande wa VIP B ni 20,000, (Buku 20 pekee) na ile VIP A ikiwa ni 30,000, (Buku 30).

Fainali hiyo itachezwa majira ya saa 10:00 jioni na mabingwa watetezi wa taji hilo ni Simba ambao walitwaa taji hilo kwa kucheza mchezo wa fainali na Namungo msimu uliopita.

SOMA NA HII  SHIRIKISHO NI MWADUI V YANGA, SIMBA V DODOMA JIJI