Home Habari za michezo YANGA WALIPIZA KISASI KWA SIMBA…WAMTAMBULISHA MZAMBIA WAO KAMA WALIVYOFANYIWA JANA….

YANGA WALIPIZA KISASI KWA SIMBA…WAMTAMBULISHA MZAMBIA WAO KAMA WALIVYOFANYIWA JANA….


Klabu ya Yanga imeendelea kuboresha kikosi chake kuelekea msimu ujao baada ya kufanikiwa kupata saini ya mshambuliaji Lazarous Kambole kutoka Kaizer Chief ya nchini Afrika Kusini.

Mabingwa hao wa msimu huu wameshinda kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji huyo wakiizidi ujanja Zesco United na kumnasa Mzambia huyo kwa mkataba wa miaka miwili.

Kambole (28) ambaye ni moja ya wachezaji wa Zambia wenye uwezo mkubwa kucheza nafasi zaidi ya mbili kwa maana ya kiungo mshambuliaji na Mshambuliaji wa kati kutokana na kocha atakavyompanga licha ya kwamba akiwa Kaizer alionekana zaidi akicheza kama mshambuliaji.

Ujio wa nyota huyo unaongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji la timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao inayoongozwa na Fiston Mayele mwenye mabao 16 kwenye Ligi Kuu Bara.

Kitendo cha Yanga kumtambulisha Kambole usiku ni kama kulipiza kisasi kwa Simba ambao nao walimtambulisha Moses Phiri muda huo huo ambao Yanga walikuwa wanasherekea ushindi wao.

SOMA NA HII  BAADA YA SIMBA KUPATA SARE JANA...AHMED ALLY AIBUKA NA KULIA NA HILI..."YAMETUACHA NA HUZUNI..WANAMASONONEKO"...