Home Habari za michezo BREAKING NEWS:….YANGA WAANIKA KIFAA CHA KAZI LEO….NI ‘ZIDANE’ WA AFRIKA…JAMAA NI BALAAH..

BREAKING NEWS:….YANGA WAANIKA KIFAA CHA KAZI LEO….NI ‘ZIDANE’ WA AFRIKA…JAMAA NI BALAAH..

Habari za Yanga

Klabu ya Yanga SC imekamilisha Usajili wa Kiungo Mshambuliaji fundi wa Kimataifa wa Ivory Coast na Klabu ya ASEC Mimosas, Zouzoua Pacome ‘Zinadine Zidane’ kwa Mkataba wa Miaka miwili.

Taarifa iliyotolewa na Yanga imeeleza;

Kuna usajili, halafu kuna usajili mkubwa. Wanachofanya uongozi wa Young Africans Sports Club kwenye dirisha hili la usajili, ni kufanya usajili mkubwa.

Ilianza kwa Nickson Kibabage, Jonas Mkude, Gift Fred, Yao Kouassi, Maxi Nzegeli, akaja Skudu, na leo uongozi wa Mabingwa wa Kihistoria Nchini umekamilisha usajili mkubwa wa kiungo Pacome Zouzoua kutoka Asec Mimosas.

Kiungo huyo wa Kimataifa kutoka Ivory Coast amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.

Pacome ameondoka Asec akiwa na rekodi ya kuwa mchezaji bora wa kikosi hiko na akifanikiwa kushinda tuzo ya Mchezaji bora wa msimu wa Ligi Kuu ya Ivory Coast ‘MVP’ msimu wa 2022/23.

Ndani ya msimu wa 2022/23, Pacome aliyeanza maisha yake ya soka kwenye timu ya vijana ya Sparta Prague ya Jamuhuri ya Czech, amefunga mabao 7 na kutoa Asisti za mabao 4.

Vilevile, Pacome amepita kwenye timu tofauti tofauti ikiwemo, SC Gagnoa, Daugavpils, Africa Sports kabla ya kutua Asec Mimosas msimu wa 2021/22.

SOMA NA HII  ENDELEA KUNUFAIKANA BONASI ZA KUTOSHA KUPITIA CZAZY JELLY YA MERIDIANBET...