Home Habari za michezo KUTOKANA NA HALI YA YANGA ILIVYO JOB AJA NA KAULI HII KWA...

KUTOKANA NA HALI YA YANGA ILIVYO JOB AJA NA KAULI HII KWA WADAU NA MASHABIKI

Habari za Yanga

Beki wa kati wa Yanga SC, Dickson Job amewomba mashabiki na wapenzi wa klabu yao, kuwaombea dua kwani bado wanayo nafasi ya kufanya vizuri katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Job ametoa kauli hiyo leo Desemba 5, 2023 walipokuwa njiani kuelekea nchini…kuwafata Medeama.

“Mashabiki watuombee, bado tunayo nafasi ya kufanya vizuri katika michezo iliyosalia, tutakwenda kupambana ili tupate matokeo,” alisema Job.

Yanga wamesaliwa na michezo minne ya Makundi baada ya kucheza miwili ambapo wamepoteza mmoja 3-0 dhidi ya CR Beloizdad na mwingine wamepata sare ya 1-1 dhidi ya Al Ahly.

Kwenye kundi lao, Yanga ndio wanaoshika mkia huku kundi lao likiongozwa na Al Ahly mwenye alama 4.

SOMA NA HII  HII HAPA VUNJA MWAKA YA MEPEMA....JAMAA KALAMBA MIL 550 ZA MERIDIANBET CASINO....