Home Habari za michezo JEAN BALEKE AJIVISHA MABOMU ATOA KAULI NZITO KWA MASHABIKI WA SIMBA

JEAN BALEKE AJIVISHA MABOMU ATOA KAULI NZITO KWA MASHABIKI WA SIMBA

Habari za Simba SC

Mshambuliaji kutoka DR Congo Jean Baleke amewashusha presha Mashabiki na Wanachama wa Klabu ya Simba SC kwa kusema bado wana nafasi ya kusonga mbele kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika watakapoenda kusaka alama tatu dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco.

Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Simba SC wakati wa Dirisha Dogo msimu uliopita 2022/23, amesema hadi sasa wana pointi mbili na wanaimani kubwa ya kupata pointi mchezo dhidi ya wenyeji wao, Wydad Casablanca ugenini ili waweze kufikisha pointi tatu muhimu kwa ajili ya kufikia malengo yao.

Baleke amewaomnba msamaha Mashabiki na Wanachama wa Simba SC kwa matokeo ya nyuma na kuwataka kuungana kuwa nguvu mmoja kuelekea kwenye mechi hiyo dhidi ya Wydad Casablanca.

Amesema wachezaji wanatambua umuhimu wa mchezo huo, na kwamba wanahitaji kufanya vizuri kwa sababu malengo yao ni kuona Simba SC inasonga mbele kuvuka makundi na kucheza Robo Fainali.

“Samahani mashabiki wetu, tusahau matokeo yaliyopita ambayo kocha wetu (Abdelhak Benchikha) amefanyia kazi mapungufu yetu sasa nguvu na akili zetu tumezielekeza kusaka ushindi dhidi ya Wydad Casablanca,” amesema Baleke.

Kuhusu tetesi za kutakiwa kurejea katika klabu yake ya TP Mazembe, Baleke amesema bado yupo na ni mtoto wa Simba, anachokifikiria zaidi ni kuona timu yake inafanikiwa kuvuka katika hatua ya makundi na kwenda robo hatimaye nusu fainali.

Simba SC wanatarajia kushuka dimbani Desemba 9, mwaka huu, wakiwa ugenini dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco, mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa Grand stade de Marrakech, uliopo Marrakech, saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

SOMA NA HII  BENCHIKHA: NIWAKUTE NYOTA WOTE KAMBINI