Home Simba SC KONDE BOY AANDALIWA MAALUMU KWA AJILI YA KAZI KESHO KWA MKAPA

KONDE BOY AANDALIWA MAALUMU KWA AJILI YA KAZI KESHO KWA MKAPA


KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes, amesema kwamba anaelewa uzito wa mechi yao dhidi ya Al Merrikh kiasi cha kuamua kumuandaa kiungo wake mshambuliaji, Luis Miquissone, ‘Konde Boy’ kwa ajili ya kuwamaliza Wasudan hao.

Kesho, Machi 16 Simba itawakaribisha wapinzani wake hao kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya makundi.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Al Hilal, dakika 90 ubao ulisoma Al Merrikh 0-0 Simba na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

Ikiwa inaongoza kundi A na pointi zake 7 mchezo wa kwanza ilishinda mbele ya AS Vita ugenini bao 1-0 na ule wa pili ilishinda bao 1-0 dhidi ya Al Ahly, Uwanja wa Mkapa na mfungaji alikuwa ni Luis.

 

Kocha huyo ameongeza kwamba, anamuandaa Luis ambapo kwa sasa ameamua kumpa program ya kupumzika kwa ajili ya kumfanya awe fiti kwa asilimia 100 ili atimize jambo hilo.

“Luis amechoka ndio maana tunampumzisha ili aweze kuwa fiti kwa asilimia 100, amekuwa akijitoa kwa ajili ya timu na hilo lipo wazi akishirikiana na wachezaji wenzake ndani ya timu.


“Ni muhimu kwa wachezaji wote kuweza kupata muda wa kupumzika ili kuwa sawa kwa ajili ya mchezo wetu ambao hautakuwa mwepesi ndani ya dakika 90,” .

 

SOMA NA HII  SIMBA YAWASHUSHIA AL AHLY BEI YA KUMPATA LUIS..SASA WANATAKA 650K TU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here