Home Habari za michezo KILICHOPO NYUMA YA PAZIA ISHU YA JEZI ZA VUNJA BEI NA POLISI...

KILICHOPO NYUMA YA PAZIA ISHU YA JEZI ZA VUNJA BEI NA POLISI TANZANI….WAAMUA KUCHUKUA MAAMUZI MAGUMU…


Mabosi wa Polisi Tanzania FC wamethibitisha kuachana na mdhamini wao upande utengenezaji na usambazaji wa wa jezi Kampuni ya Vunjabei.

Katika mchezo dhidi ya Yanga uliopigwa Jumanne ya wiki hii, jijini hapa na timu hiyo ilifungwa mabao 2-1, Polisi ilitumia jezi ambazo hazina nembo hata ya mdhamini mmoja.

Ulipotafutwa Uongozi wa timu hiyo kujua kulikoni, ndipo Makamu Mwenyekiti, Robert Munisi alisema walitumia jezi zisizo na nembo ya mdhamini kwani wamemaliza mkataba na Vunjabei waliokuwa wakiwavisha, ila jezi mpya zipo njiani na zitatambulishwa kwa mashabiki wao.

“Tumemaliza mkataba na Vunjabei na sasa hivi tunavalishwa na Masita, ila jezi ndio zimechelewa kufika ila tunatarajia hivi karibuni zitafika,” alisema Munisi.

Aliongeza mkataba wao na Vunja Bei ilikuwa wa mwaka mmoja na baada ya kumalizika hawajaona haja ya kuendelea nao ikabidi wasaini mkataba mpya na Masita na kuthibitisha kwamba jezi ziko njiani kutoka Uholanzi.

Kuhusu mdhamini mkuu alisema bado anabaki ni yule yule Lodhia hivyo wadau na mashabiki wao wala wasiwe na wasiwasi kila kitu kitakuwa sawa na mara hii wamepanga kuwaletea jezi zenye hadhi ya Timu ya Polisi Tanzania FC..

SOMA NA HII  YANGA WAIFANYIA UMAFIA SIMBA KWENYE DILI LA MANZOKI...NABI AINGILIA MCHEZO NA KUHARIBU MAMBO USIKU USIKU...