Home Habari za michezo KISA KIPIGO TOKA IHEFU JANA….GAMONDI ATAJA ALIYEIMALIZA YANGA…

KISA KIPIGO TOKA IHEFU JANA….GAMONDI ATAJA ALIYEIMALIZA YANGA…

Habari za Yanga SC

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Angel Gamond ametaja sababu ya kupoteza mechi yao dhidi ya Ihefu FC, yakiwemo makosa yaliyofanywa na safu ya ulizi na kama timu kutotumia vizuri nafasi wanazotengeneza.

Yanga walikuwa ugenini katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa juzi Uwanja wa Highland Estate, uliopo Ubaruki Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, kuendeleza uteja mbele ya wenyeji Ihefu FC kwa dakika 90 kukamilika kwa matokeo ya mabao (2-1).

Gamond alisema wapinzani wao walitumia makosa machache kwenye safu ya ulinzi na timu ilishindwa kutumia nafasi walizozitengeneza na wala sio kwa sababu ya muamuzi .

Alisema muamuzi wa mchezo hakutenda haki maana kuna maamuzi yalikuwa yanawaumiza, kuna wakati wakiwa kwenye mwendo kuelekea kwa wapinzani alikuwa anapuliza filimbi.

“Hali hiyo imekatisha tamaa kwa wachezaji wangu, siwezi kuwatupia lawama waamuzi kwa sababu walifanya majukumu yao na wachezaji walishindwa kutumia nafasi walizozitengeneza na kuweza kufanga huku safu ya ulinzi ikifanya makosa.

Kumetokea changamoto nyingi kwenye mechi ya leo (juzi), wengine wamepoteza muda lakini muamuzi alikuwa na jukumu la kuzuia hayo lakini hatuwezi kusema tumefungwa kwa ajili ya makosa yake, tunapaswa kuchukua lawama za kupoteza mchezo huu,” alisema Gamond.

Aliongeza kuwa alifanya mabadiliko mengi kwenye mechi lakini kipindi chote cha kwanza waliweza kucheza vizuri ni kosa la kawaida kwenye mechi lililofanywa na Djigui Diarra lakini kipindi cha pili wachezaji hawakucheza vizuri.

Kocha huyo alisema wanasahau matokeo ya mchezo huo na kujipanga na mechi yao ijayo kuhakikisha wanafikia kupata matokeo mazuri ikiwa mchezo huo wanacheza ugenini.

Naye Kocha wa Ihefu FC, Zuberi Katwila, alisema aliiangalia Yanga jinsi wanavyocheza na kuwaandaa wachezaji wake wanakuwa imara muda wote na kuziba njia zote ambazo zingeweza kupata ushundi.

Alisema kikubwa ni pointi tatu au moja, haikuwa mechi rahisi, walicheza kwa tahadhari kubwa na kuwaheshimu sana Yanga na kutumia makosa yao kupata alama walizohitaji katika mchezo huo.

“Niliwapa tahadhari kubwa wachezaji wangu ubora wa safu ya ushambuli wa Yanga unatoka na mipira kutoka kwa viungo na tulifanikiwa kubana katika maeneo yao na kuzuia njia zote za kupata ushindi nalo tulifanikiwa.

“Mabadiliko ya kikosi yameweza kunisaidia kwa sababu kuna wachezaji mechi iliyopita Saadun na Never Tigere walianzia benchi ikiwa ( Super Sub) leo nimewaanzisha ili kutafuta ushindi baadae niliwatoa na kuwaweka wengine na kuimarisha safu yangu ya ulinzi baada ya kuona washambuliaji wangu kufanya kazi vizuri ,” alisema kocha huyo.

Aliwapongeza nyota wake kwa kuhakikisha wanafuata alichowaelekeza na kupata pointi tatu, kwa sababu haikuwa mechi rahisi kucheza na Yanga na kufanikiwa kupata ushindi na sasa wanaenda kutafuta pointi muhimu ugenini dhidi ya KMC FC.

SOMA NA HII  KAMA ILIKUPITA ,...HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA JANA MGUNDA AKIBEBA TUZO NA 'MAPESA' ....