Home Habari za michezo KAMA ILIKUPITA ,…HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA JANA MGUNDA AKIBEBA TUZO NA ‘MAPESA’ ….

KAMA ILIKUPITA ,…HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA JANA MGUNDA AKIBEBA TUZO NA ‘MAPESA’ ….

Kocha Mkuu wa Simba SC, Juma Mgunda amekabidhiwa tuzo ya kocha bora wa Ligi Kuu ya NBC mwezi Novemba muda mfupi kabla ya kuanza mchezo  dhidi ya Geita Gold kuanza katika Uwanja wa CCM Kirumba ambao ulimalizika kwa Siba SC kuibuka na ushindi wa magoli 5.

Mgunda aliwashinda makocha Hans Van Pluijm wa Singida Big Stars na Meck Mexime wa Kagera Sugar ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Katika mwezi Novemba Mgunda ameiwezesha Simba SC kushinda mechi nne dhidi ya Ihefu, Namungo, Ruvu Shooting na Polisi Tanzania huku akitoka sare dhidi ya Mbeya City na Singida Big Stars.

Hii ni mara ya kwanza kwa Mgunda kushindika tuzo ya kocha bora wa mwezi tangu ajiunge na Simba SC  Septemba mwaka huu.

Mgunda amekabidhiwa tuzo hiyo na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mguto pamoja na  mfano wa hundi ya Sh. 1,000,000.

SOMA NA HII  AL MAREIKH WAJA NA MATOKEO YAO HAYA DHIDI YA YANGA